Kufikia Lengo
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Wafilipi 3:10-12 Ili nimjue yeye, na uweza wa kufufuka kwake, na ushirika wa mateso yake, nikifananishwa na kufa kwake; ili nipate kwa njia yo yote kuifikia kiyama ya wafu. Si kwamba nimekwisha kufika, au nimekwisha kuwa mkamilifu; la! Bali nakaza mwendo ili nipate kulishika lile ambalo kwa ajili yake nimeshikwa na Kristo Yesu.
Kuna udanganyifu mkubwa kuliko wote ambao Shetani amepandikiza katikati ya watu wa Mungu. Ni kwamba, mtu anaweza kuokoka na kupokea karama ya uzima wa milele bure bila kuwa na mabadiliko maishani mwake.
Sasa, kama umeshajua lolote kuhusu Habari Njema za Yesu, labda utaniuliza.., unasemaje? Je! Ni lazima nifanye kazi ili nipate fadhili mbele za Mungu? Hapana, si hivyo hata kidogo! Jana tu, tulisikia alivyosema Mtume Paulo:
Wafilipi 3:9 … nionekana katika yeye, nisiwe na haki yangu mwenyewe ipatikanayo kwa sheria, bali ile ipatikanayo kwa imani iliyo katika Kristo, haki ile itokayo kwa Mungu, kwa imani.
Hii ndiyo Habari Njema, lakini mtu asipoiishi imani hiyo, basi atakuwa hajapokea kweli-kweli karama ya neema inayotolewa ndani ya Kristo. Tuendelee kusoma hapo hapo:
Wafilipi 3:10-12 Ili nimjue yeye, na uweza wa kufufuka kwake, na ushirika wa mateso yake, nikifananishwa na kufa kwake; ili nipate kwa njia yo yote kuifikia kiyama ya wafu. Si kwamba nimekwisha kufika, au nimekwisha kuwa mkamilifu; la! Bali nakaza mwendo ili nipate kulishika lile ambalo kwa ajili yake nimeshikwa na Kristo Yesu.
Lengo hasa alilokuwa nalo Kristo wakati alipokufanya uwe wake ni kubadilisha maisha yako, na huwa inatokea pale mtu anaposhiriki mateso yake. Wewe na mimi, hatujawa vile Mungu anavyotamani tuwe, Lakini tuko njiani kwenye safari ya mabadiliko, angalau ingetupasa kuwa tumeshaanza safari hiyo.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.