Kuhesabiwa Haki kwa Imani
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Warumi 5:1 Basi tukiisha kuhesabiwa haki itokayo katika imani, na mwe na amani kwa Mungu, kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo.
unapotenda yasiyo haki huwa unajaribu kujitetea mbele za watu wengine..Huko ni kujihesabia haki, ni lazima tujiulize ….kwanini tunafanya hivyo?
Ni swali linalovutia, Kwanini tunajitetea na kujihesabia haki tunapofanya kosa? Ni kwasababu, tunavutwa na hali ya kutenda mema. Tunataka kujiona na kuonekana mbele za watu wengine kwamba tumetenda mema, hata kama si kweli.
Kwanini tunasimulia habari hii siku hizi tukikaribia Pasaka? Ni kwasababu karama iliyotoka kwenye msalaba pale Kristo alipomwaga damu yake; ni kuhesabiwa haki: Sikiliza:
Warumi 5:1 Basi tukiisha kuhesabiwa haki itokayo katika imani, na mwe na amani kwa Mungu, kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo.
Ukiona neno “basi” katika Maandiko, lazima ujiulize, kwa nini “basi” imeandikwa hapo? Kwa mstari huu, mwandishi ambaye ni Mtume Paulo anarudisha mawazo yetu kwa sura zilizotangulia, pale alipoeleza namna mtu, ameweka imani yake ndani ya kazi ambayo Yesu alitufanyia pale msalabani, dhambi zake zinasamehewa kabisa kwasababu dhabihu yake Kristo ililipa gharama iliyodaiwa na haki ya Mungu.
Tukifanya kosa, hatuwezi kuwa na amani tena, si kweli? Ndiyo maana tunaamua kupitia njia ya kujihesabia haki, tukijaribu kurejesha ile amani, tukijiweka upande wa haki. Ukitaka kujua ukweli, tuna hamu ya kuhesabiwa haki, kuwa na msimamo sahihi na kupata amani inayoendana na hali hiyo.
Lakini kama tunataka kuhesabiwa haki kweli kweli, na kuwa na msimamo sahihi mbele za Mungu na kupata amani ya kweli … kuna njia moja tu. Ni kuweka imani yetu ndani ya Yesu, aliyelipa deni la dhambi zetu.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.