... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Simama Kidete

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Yakobo 3:10-12 Katika kinywa kile kile hutoka baraka na laana. Ndugu zangu, haifai mambo hayo kuwa hivyo. Je! Chemchemi katika jicho moja hutoa maji matamu na maji machungu?

Listen to the radio broadcast of

Simama Kidete


Download audio file

Kama tulivyoona mapema wiki hii, Yesu alisema kwamba kutoka kinywani mwake, mtu hunena yale yaujazayo moyo wake.  Ni kweli.  Yale tunayowaambia watu wengine – yakiwa mema au mabaya – yanadhihirisha yaliyomo moyoni mwetu.

Sisi sote tungependa kufikiri kwamba tuna moyo safi, kila siku ya maisha yetu, tunajaribiwa ili tusiwe na moyo safi. Kwa hiyo tunarudia hali ya kuwatendea visivyo, au hatufikii kile kiwango tunachotakiwa kuwatendea wengine kama Mungu anavyotaka. Yamkini leo ni siku ya  mwafaka wa kusimama kidete. 

Yakobo 3:10-12  Katika kinywa kile kile hutoka baraka na laana.  Ndugu zangu, haifai mambo hayo kuwa hivyo.  Je!  Chemchemi katika jicho moja hutoa maji matamu na maji machungu?  Ndugu zangu, Je!  Mtini waweza kuzaa zeituni, au mzabibu kuzaa tini?  Kadhalika chemchemi haiwezi kutoa maji ya chumvi na maji matamu. 

Je!  Wewe ni chemchemi nzuri ukiwa na maji matamu, au chemchemi mbaya itoayo maji machungu?  Je!  Wewe ni mtini au mzeituni?  Wewe ni maji ya chumvi au maji ya kunywa?  Rafiki yangu, Yesu alikufa ili upate kusamehewa dhambi zako, alifufuka tena akupe ushindi dhidi ya dhambi ili uweze kuenenda katika upya wa uzima. 

Je!  Leo itakuwa siku yako ya kudai ushindi ule?  Je!  Leo ni siku utakayosalimu amri na kuruhusu nguvu ya Roho Mtakatifu ikutakase?  Je!  Leo ni siku utakaosimama kidete na kukata shauri la kuchagua, tangu sasa hadi maisha yako yote, kuishi katika ushindi wa msalaba . Utaamua nini? 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.


We use cookies to improve your browsing experience, analyse site traffic & personalise content, but we do not track you when you leave this site. To find out how we utilise & protect your data, check out our "Privacy Policy".

Privacy Policy

Make your gift monthly to share more Living Hope!

Hearts are open to Jesus at Easter. Your monthly support will help reach millions around the world to share the hope of Christ.

Make it Monthly