Kuipata Neema
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Luka 2:16 Wakaenda kwa haraka wakamkuta Mariamu na Yusufu, na yule mtoto mchanga amelala horini.
Sijui ikoje kwako, lakini kwangu mimi neema ya Mungu bado inanishangaza sana. Pia, kadiri ninavyojaribu kupokea ukweli wa neema ya Mungu pamoja na rehema zake na upendo wake kwangu ndani ya Yesu, ndivyo unazidi kutokueleweka.
Kwanini muitikio wangu uko hivi?…Ni kwa sababu kwa upande mmoja ninaona yote aliyonitendea. Lakini kwa upande mwingine ninaona uasi wangu, dhambi zangu, nikijua ya kwamba ninavyostahili ni hukumu ya Mungu tu. Sisi sote tunafanana. Hatufikii utukufu wa Mungu.
Kwa miaka mingi, silika yangu ilikuwa ni kukimbia mbali na Mungu. Kujificha. Lakini silika ya wale wachungaji waliokaa kondeni usiku ule, wakati malaika wanawaambia Habari Njema ya kuzalikwa kwa Mwokozi wao … silika yao ilikuwa kumkibilia Mungu.
Luka 2:16 Wakaenda kwa haraka wakamkuta Mariamu na Yusufu, na yule mtoto mchanga amelala horini.
Halafu ndani ya zizi lile, ndani ya hori lile, sehemu chafu ya mifugo, waliikuta neema ya Mungu yenye utukufu, unyenyekevu na upole pia.
Kuna vipindi katika maisha yetu dhambi zetu ni zinakuwa nyingi, ndio maana tunataka kukimbia. Yaani tunasisitizwa kwa nguvu kumpa Mungu kisogo na kumkimbia, Hali hiyo inatokana na dhambi. Lakini rafiki yangu, ujue kwamba, Yesu alikuja kwa ajili yako! Kristo alikuja ili awe Mwokozi wako.
Umrudie. Gundua neema yake. Gundua pendo kuu lililosababisha Mungu amtume Mwanae wa pekee duniani kwa unyenyekevu mkubwa ili ateswe na kufa kwa ajili yako ili dhambi zako zipate kusamehewa.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.