... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Kutafuta Neema

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Luka 2:16 Wakaenda kwa haraka wakamkuta Mariamu na Yusufu, na yule mtoto mchanga amelala horini.

Listen to the radio broadcast of

Kutafuta Neema


Download audio file

Kwa kweli, Krismas ni kipindi cha ajabu sana, Krismas ni sikukuu maalum.  Lakini hata hivyo kuna wengine wanaifanya kuwa ya kawaida tu. Ukiangalia, sisi sote tumesherehekea Krismas mara nyingi sana kwa hiyo hatusisimki tena.

Ni kweli, Kwa watu wengi, hata Wakristo baadhi, Krismasi ni sikukuu ya kumpumzika kazi na kutulia siku moja, mbili.  Tunafahamu maana yake kwamba Yesu alizaliwa pale wanapolaza mifugo kwa sababu hapakuwa na nafasi kwenye nyumba za kulala wageni,  Tunafahamu hayo yote.  Tusichangamke kupita kiasi, bali tutulie, tupumzike, tule wali na nyama tukitumia na soda, basi. 

Je!,  Hayo ndiyo unayoyafikiria tu kuhusu Krismas?  Nguo na wali?

Hivi karibuni tumeongelea kuhusu neema ya Mungu iliyodhihirika pale alipomtuma Yesu ulimwenguni.  Wale wachungaji kondeni walikutana na jeshi la malaika angani wakiimba Hosanna, hosanna juu mbinguni. 

Yaani zilikuwa taarifa za ajabu-ajabu katika maisha yao, wale wachungaji walipozisikia.  Kwanza waliduaa, lakini baada ya kutafakari kidogo, walifanyeje?  Habari njema hii waliifanyia nini? 

Luka 2:16  Wakaenda kwa haraka wakamkuta Mariamu na Yusufu, na yule mtoto mchanga amelala horini. 

Wale wachungaji walikimbilia neema ya Mungu.  Masihi wao alikuwa amezaliwa. Huu ndio msukumo wa Habari Njema mioyoni mwao.  Na walimkuta Mwokozi wao amelala ndani ya hori chafu ya kulia ng’ombe.  Ni sehemu Mungu aliyochagua kudhihirisha neema yake isiyoelezeka kwetu,.  Yesu alilazwa ndani ya hori la kulia ng’ombe. 

Kwahiyo usikae kwenye mazoea yako ya kawaida.  Simama.  Kimbia.  Kimbilia neema ya Mungu , neema isiyoelezeka.  Yesu. 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.