Kujinyenyekesha
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Yakobo 4:8-10 Mkaribieni Mungu, naye atawakaribia ninyi. Itakaseni mikono yenu, enyi wenye dhambi, na kuisafisha mioyo yenu, enyi wenye nia mbili. Huzunikeni na kuomboleza na kulia. Kucheka kwenu na kugeuzwe kuwa kuomboleza, na furaha yenu kuwa hamu. Jidhilini mbele za Bwana, naye atawakuza.
Wiki hii tumekuwa tuna masimulizi kuhusu ukubwa, ukubwa halisi. Sio ukubwa bandia unaotolewa na utamaduni wetu unaotafuta umaarufu, hapana; lakini ukubwa unaoweza kutikisa maisha ya watu wengine hadi milele.
Je! Utaniruhusu leo nikikuuliza, Maisha yako yakifikia ukomo wake, Je! Itakuwa imetikisa maisha ya watu wengine hadi milele? Kwa sababu kama wewe ni mtu aliyemwamini Yesu, ndiyo hayo aliyokuagiza uyafanye.
Lakini tunawezaje kufanya hivyo? Sisi sote tu wenye dhambi. Sisi sote, tukiangalia kwenye kioo tutaona madhaifu yetu, upungufu wetu, na jinsi tumefeli. Nimejitahidi kwa kweli, lakini naona sileti mabadiliko yo yote.
Hisia kama hii ni kawaida. Sasa Mungu anaionaje? Tunawezaje kutatua kitendawili hicho kisirudi tena?
Yakobo 4:8-10 Mkaribieni Mungu, naye atawakaribia ninyi. Itakaseni mikono yenu, enyi wenye dhambi, na kuisafisha mioyo yenu, enyi wenye nia mbili. Huzunikeni na kuomboleza na kulia. Kucheka kwenu na kugeuzwe kuwa kuomboleza, na furaha yenu kuwa hamu. Jidhilini mbele za Bwana, naye atawakuza.
Jibu ni kumkaribia Mungu tu, kupitia maombi na kusoma Neno lake, kustawisha uhusiano mzuri kama alivyokusudia. Usiwe na nia mbili, kana kwamba unaweza kufuata na kutafuta mambo ya dunia hii na bado kuwa na mahusiano mazuri na Mungu. Haiwezekani jamani.
Jidhilini mbele za Bwana, naye atawakuza.
Rafiki yangu, Mungu amekusudia kubadilisha ulimwengu huu, kwa kubadilisha nafsi moja moja … kupitia wewe.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.