Kujua Mapenzi Ya Mungu
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
2 Timotheo 3:16,17 Kila andiko, lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaabidisha katika haki; ili mtu wa Mungu awe kamili, amekamilishwa apate kutenda kila tendo jema.
Ungonjwa mmoja mbaya uliopo kati ya watu wa Mungu sehemu nyingi duniani ni kukosa kujua Neno lake. Kwa upande mmoja, watu wana shauku kutambua mapenzi ya Mungu kwa ajili ya maisha yao. Lakini kwa upande mwingine, wanaacha Biblia zao kwenye shelfu zikizidi kukusanya vumbi.
Ni ajabu sana. Wakristo wanaoteswa vibaya, na baadhi yao hawana hata Biblia, wanafahamu Neno la Mungu vizuri na kulikumbatia kuliko wale wenye uhuru wa kuabudu.
Zamani wakati nilikuwa mwanafunzi kwenye chuo cha Biblia, tulikuwa na mwalimu mmoja aliyewahi kuwa mchungaji zaidi ya miaka thelathini. Yeye alisema wakati alihamia kwenye kanisa lingine, aliwachukulia wanakanisa kuwa ni wajinga katika kuijua Biblia. Kinachohuzunisha ni kwamba, kila mahali aliona kwamba ndivyo walivyokuwa.
Je! Utaniruhusu nikikuuliza habari ya ujuzi wako wa Biblia? Je! Moyo wako na mawazo yako yamezama kiasi gani katika Maandiko? Kwa sababu …
2 Timotheo 3:16,17 Kila andiko, lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaabidisha katika haki; ili mtu wa Mungu awe kamili, amekamilishwa apate kutenda kila tendo jema.
Kikwazo kikubwa kuliko vyote kinachozuia mtu asiishi maisha ya utaua, maisha ya amani na uwezo, maisha yenye furaha na kuhudumia wengine ni dhambi zake zenyewe. Ni kweli kabisa! Sasa dawa na kinga ya hali hiyo ni uwezo uliomo katika Neno la Mungu, uwezo wa kubadilisha maisha yetu.
Huwezi kugundua mapenzi ya Mungu kwako kama wewe unabaki kuwa mjinga usilijue Neno lake.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.