Upanga Ukatao Kuwili
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Mithali 10:2-4 Hazina za uovu hazifaidii kitu; bali haki huokoa na mauti. BWANA hataiacha nafsi ya mwenye haki ife na njaa; bali tamaa ya mtu mwovu huisukumia mbali. Atendaye mambo kwa mkono mlegevu huwa maskini; bali mkono wake aliye na bidii hutajirisha.
Kuna ukinzani mkubwa katika ulimwengu huu, kwamba kila kilicho chema kinaweza kugeuzwa kuwa kitu kibaya. Kila Baraka kwa muda mfupi tu, inaweza kugeuka kuwa laana.
Ebu fikiria kidogo, Je! pesa zenyewe ni mbaya? Inategemeana jinsi tunayotumia pesa hizo. Tukitoa pesa kwa kusaidia wahitaji, inakuwa nzuri sana. Lakini wakati mtu anatamani, wakati anaiba, wakati anakuwa bahili, pesa inakuwa kitu kibaya mno.
Je! Kufanya kazi kwa jitihada, ni jambo jema au baya? Inategemeana kama kazi hiyo ni halali au laa. Swali lingine, je! Ni lini mapumziko mazuri yanageuka kuwa uvivu? Kwa kweli, kila kitu chema kinakata kuwili kama vile upanga ukatao kuwili. Inategemeana na jinsi mtu anavyokitumia.
Mithali 10:2-4 Hazina za uovu hazifaidii kitu; bali haki huokoa na mauti. BWANA hataiacha nafsi ya mwenye haki ife na njaa; bali tamaa ya mtu mwovu huisukumia mbali. Atendaye mambo kwa mkono mlegevu huwa maskini; bali mkono wake aliye na bidii hutajirisha.
Mungu mwenyewe, anaona mali uliyo nayo kama uliipata kwa haki au kwa udhalimu. Anaona kama unatumika kwa bidii au kama wewe ni mvivu. Anafahamu makusudi ya moyo wako. Kama vile mtu fulani aliyewahi kusema, “Heri mtu yule aliyejifunza kushangilia kitu bila kuwa na tamaa, aliyejifunza kufuata wengine bila kuiga, anayeweza kusifu bila kubembeleza, anayeweza kuongoza wengine bila kuwatawala kwa hila.”
Utendapo neno lolote, fanya yote kwa moyo mweupe, kwa sababu … BWANA hataiacha nafsi ya mwenye haki ife na njaa.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.