... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Kulea Watoto Walio Imara

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Wagalatia 5:13 Mithali 23:13,14 Usimnyime mtoto wako mapigo; maana ukimpiga kwa fimbo hatakufa. Utampiga kwa fimbo, na kumwokoa nafsi yake na Kuzimu.

Listen to the radio broadcast of

Kulea Watoto Walio Imara


Download audio file

Onyo la Biblia kusema kwamba wanaokataa kutumia fimbo kwa kuwadhibu mtoto wanamharibu, ni kama haiendani na mfumo wa kisiasa wa siku hizi.  Ni kweli, kuna njia nzuri za mbadala kwa kuadhibu watoto wetu bila kuwapiga, lakini lazima tuwaadhibu.

Mimi binafsi nilishiriki katika kulea watoto watano maishani mwangu na kuna mambo mawili niliyoyagundua ambayo naweza kukwambia sasa.  Kwanza ,si kila baba mzazi ni mkamilifu,  Cha pili, kulea watoto ni kazi ngumu mno katika maisha. 

Ni kweli, kuna siku za furaha nyingi tu,  Lakini kuna siku inatakiwa mzazi awe thabiti kabisa. Lakini ni kama uwekezaji ambao karibu mara zote unaleta faida kubwa sana.  Nimependezwa sana kuona jinsi watoto wangu wamekuwa, wakiwa sasa raia wema, wenye heshima na maadili. 

Lakini matunda yale, yanatokana na jinsi ulivyowajenga  ndani yao … yaani kujenga tabia zao, na hii si kazi rahisi hata kidogo. 

Mithali 23:13,14  Usimnyime mtoto wako mapigo, maana ukimpiga kwa fimbo hatakufa.  Utampiga kwa fimbo, na kumwokoa nafsi yake na Kuzimu. 

Kama nilivyosema, ni vizuri kuwaadhibu watoto.  Mfumo wa siku hizi kuwaachilia watoto, ni kuwaharibu kabisa na bila shaka watakuwa watu wazima wasio na nidhamu wala hawatakuwa imara kwa kukabiliana na changamoto za maisha. 

Kama vile Michael Anderson wa shirika la Kulenga Familia alivyosema: “Kwa watoto wetu karibu wote, maisha yatawawia vigumu sana kuliko wanavyotazamia.  Ni wajibu wetu kuwaanda wawe imara ili waweze kukabiliana na changamoto hizo.”   

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.