Kumwita Mungu
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Zaburi 86:5 Kwa maana Wewe, Bwana, U mwema, umekuwa tayari kusamehe, na mwingi wa fadhili, kwa watu wote wakuitao.
Je! Umewahi kutenda jambo baya mno na kumwumiza mtu vibaya, mtu ambaye unampenda kiasi cha kutokuweza kufikiri kwamba unaweza kusamehewa? Unashindwa kufikiri jinsi mahusiano yenu yangeweza kupona tena lakini ghafla … unakuta mtu yule anakusamehe.
Wakati mtu anakusamehe kwa kosa ambalo unajua ni baya mno na unafahamu pia kwamba kwa kawaida usingesamehewa, kwa kweli ni hisia nzuri ya kuwekwa huru, kurejeshwa. Yaani ni hisia ambayo ni vigumu kuieleza kwa maneno. Unakosa jinsi kueleza lakini kumbe, unajikuta umesamehewa!
Nilimsikia mchezaji wa filamu aitwaye Denzel Washington akimsifia mke wake wa miaka mingi, Pauletta. Alianza kutoa machozi wakati alikuwa anamtukuza akisema hivi, “Miaka hii arobaini aliendelea kunisamehe kila siku, licha ya mapungufu yangu.”
Uwezo wa kusamehe ni kipeo cha upendo kabisa. Yaani msamaha unaupamba vizuri upendo. Ndio uliomsukuma mtunga Zaburi kuandika yafuatayo:
Zaburi 86:5 Kwa maana Wewe, Bwana, U mwema, umekuwa tayari kusamehe, na mwingi wa fadhili, kwa watu wote wakuitao.
Hailishi umefanya kitu gani, wakati unaweka tumaini lako kwake Yesu na kazi aliyokufanyia, Mungu atakidhi hitaji lako kubwa kuliko yote kupitia mafanikio yake makubwa kuliko yote. Umesamehewa.
Kwa maana Wewe, Bwana, U mwema, umekuwa tayari kusamehe, na mwingi wa fadhili, kwa watu wote wakuitao.
Na Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.