Kuona Huruma
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Yakobo 2:13 Maana hukumu haina huruma kwake yeye asiyeona huruma. Huruma hujitukuza juu ya hukumu.
Kuna maneno kadhaa katika Biblia yanasumbua kweli. Yaani maandiko mengine tungependa kuyaruka tu. Mistari unaotukwaza katika theolojia ndio tunaotaka kuuchunguza leo.
Nitangulie kwa kusema kwamba, mimi ninaamini mtu anaweza kuokolewa kwa neema ya Mungu tu, kupitia imani ndani ya Yesu aliyekufa na kulipa deni la dhambi zetu, akafufuka pia ili atupe karama bure ya uzima wa milele.
Lakini mimi siko pamoja na wale wanaofundisha kwamba mtu akiokoka ameokoka daima. Si kwamba ninajijengea theolojia yangu kuhusu mada hii, bali ni kwa sababu mtu akisoma Biblia moja kwa moja, sioni sehemu Biblia inasema hivyo:
Yakobo 2:13 Maana hukumu haina huruma kwake yeye asiyeona huruma. Huruma hujitukuza juu ya hukumu.
Kulielewa Neno la Mungu, kulisoma moja kwa moja kama lilivyoandikwa, ni njia bora. Na ukisoma mstari huu, utaona kwamba mtu anaweza kumwamini Yesu, lakini kama haonei wengine huruma, basi siku ile ya hukumu, Mungu hatamwonea huruma.
Isitoshe, Yesu alitoa mfano mzima kuhusu swala hili. Alianza kwa kusema kwamba, “Ufalme wa Mbingu unafanana na …” na alimalizia kwa habari ya mtumishi asieona hurumu kufungwa na kuteswa hadi alipe mfalme deni lake lisilobebeka.
Kwahiyo tuseme wazi kabisa. Kuonea huruma si hiari ya mtu, kukosa kuwaonea wengine huruma ni kukosa kuhurumiwa na Mungu.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.