Kuona Vizuri
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Mithali 19:11 Busara ya mtu huiahirisha hasira yake; nayo ni fahari yake kusamehe makosa.
Matusi hayaepukiki, lakini mtu akitukanwa huwa anaumia sana, sindiyo? Lakini punde tu aliyetukanwa huwa anataka kujilipiza kisasi. Lakini hapo mtu atakuwa amejiingiza sehemu ya hatari kabisa.
Inategemeana na tabia ya mtu lakini njia mojawapo ya kulipiza kisasi ni kushambulia kwa maneno kama shetani anavyofanya, mt mwingine anaweza kutafuta siku ya kujilipiza kisasi.
Wengine wanajikunja tu wakirudia rudia tusi mioyoni mwao huku wakizidi kuwa na uchungu na kuanza kutumia mbinu ya mgomo baridi.
Kwa vyovyote vile, ukiweka uchungu na hasira moyoni mwako, utakuwa umejiweka mahali pa hatari sana kwasababu huwezi kuona vizuri tena. Sijui kama umeshajaribu kuangalia sura yako kwenye sufuria ya maji iliyochemshwa? Maji yakipoa na kutulia, ndipo mtu anawezaka kuangalia vizuri na kuona sura yake. Ndiy maana kutenda jambo lolote kwa hasira ni tendo la hatari sana.
Mithali 19:11 Busara ya mtu huiahirisha hasira yake; nayo ni fahari yake kusamehe makosa.
Anachokisema Mungu katika mstari huu ni kwamba, mtu anaweza kuzoea kutumia busara kwa kuvumilia matusi. Hasemi uwe na subira kwa kutafuta muda mwafaka wa kujilipiza kisasi, hapana!. Wala hasemi mtu ajifanye mwathiriwa tu.
Subira ya ki-Mungu, Halafu kadiri mtu anavyotembea katika hekima ya KiMungu, ndivyo anavyozidi kukomaa hata kama mambo yanazidi kuwa magumu. Sasa, mtu akikomaa, haitamuwia vigumu kusamehe matusi. Acha nitaje mstari ule tena ili Roho Mtakatifu ajenge picha moyoni mwako.
Busara ya mtu huiahirisha hasira yake; nayo ni fahari yake kusamehe makosa.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.