Kuondoa Mzigo Mzito
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Matendo 3:19 Tubuni basi, mrejee, ili dhambi zenu zifutwe, zipate kuja nyakati za kuburudishwa kwa kuwako kwake Bwana.
Sisi sote tunabeba mizigo maishani na kuna wengine mizigo yao ni mizito ni mno. Wengine labda si mizito sana lakini hata hivyo mizigo iliyopo inaweza kumlemea mtu hata asiweze kupiga hatua wala kukimbia mbio; yaani mizigo huwa inasababisha mtu kutembea kwa kujivuta.
Halafu kadiri mtu anavyoendelea kubeba mizigo, ndivyo inavyomuwia vigumu zaidi. Kuna wimbo wa zamani unaoanza na maneno yafuatayo: Nani aweza kuniweka huru? (na mzigo wa dhambi).
Pengine hujawaza kwamba dhambi zako, mapungufu yako, madhaifu yako na kushindwa kwako – ni “mzigo” lakini kwa kweli hayo yote ni mizigo. Ni kama chuma cha risasi ndani ya begi unayoibeba na kweli begi litazidi kukulemea kadiri risasi ile ya dhambi inavyoongezeka kila siku.
Kwahiyo, tuulize, Je!, Jibu litapatikana wapi?, Mtu akichoka kuna swali nyeti analopaswa kuliuliza, Je! Nawezaje kutupa chini risasi hiyo? Ninawezaje kupunguza uzito wa mzigo wangu? Basi, sikiliza jibu la swali lako:
Matendo 3:19 Tubuni basi, mrejee, ili dhambi zenu zifutwe, zipate kuja nyakati za kuburudishwa kwa kuwako kwake Bwana.
mmmh, neno “tubuni” … kumbe linasikika kuwa neno la kidini lililopitwa na wakati. Lakini maana yake ni kubadilisha mawazo yako kabisa na kumgeukia Mungu; kukata shauri moja kwa moja kwamba dhambi zile hazifai hata kidogo.
Halafu, ukifanya hivyo, ukirejea na kutulia mbele za Mungu … uwepo wake tu ndio utakuletea burudisho. Je!, Hayo sindiyo tunayoyataka sisi sote?
Tubuni basi, mrejee, ili dhambi zenu zifutwe, zipate kuja nyakati za kuburudishwa kwa Bwana.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.