... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Mambo Mungu Aliyoyaandaa

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

1 Wakorintho 2:9,10 Lakini kama ilivyoandikwa, Mambo ambayo jicho halikuyaona wala sikio halikuyasikia, (wala hayakuingia katika moyo wa mwanadamu,) mambo ambayo Mungu aliwaandalia wampendao. Lakini Mungu ametufunulia sisi kwa Roho. Maana Roho huchunguza yote, hata mafumbo ya Mungu.

Listen to the radio broadcast of

Mambo Mungu Aliyoyaandaa


Download audio file

Ni ajabu namna mkusanyiko wa mambo madogo madogo – yanayotusumbua pamoja na matazamio ya wengine yanakua na kuwa makubwa kwenye maisha yetu.

Haieleweki wala tusingetamzia  namna maisha yanavyoweza kuanza kutubana taratibu taratibu bila sisi kujua kinachoendelea hadi siku ile mtu anajikuta ameleemewa sana. Halafu siku moja unaamka na kujiuliza, “Kwanini ninachoka hivi?”  Ikifikia hapo, yale mema yote uliyoyatazamia, uzuri na mshangao katika maisha yako, vyote ni kama vimetoweka. 

Ninaamini kwa moyo wangu wote kwamba leo hii, Mungu anataka kukuita tena urejee katika uzuri wake, mshangao wa kazi zake na mpango wake wa ajabu kwa ajili yako.  Si kwa kupitia yale ninayoyasema mimi lakini kwa kupitia yale yeye mwenyewe asemayo akikwambia moja kwa moja:

1 Wakorintho 2:9,10  Lakini kama ilivyoandikwa, Mambo ambayo jicho halikuyaona wala sikio halikuyasikia, (wala hayakuingia katika moyo wa mwanadamu,) mambo ambayo Mungu aliwaandalia wampendao.  Lakini Mungu ametufunulia sisi kwa Roho.  Maana Roho huchunguza yote, hata mafumbo ya Mungu. 

Anachosisitiza ni kwamba, siri ya uzuri na mshangao wa Mungu umefichwa machoni pa watu wa ulimwengu. Lakini kadiri Roho wake Mtakatifu anachukua Neno lile na kulidhihirisha ndani ya mioyo yetu, ghafla … tunasisimka!  

Rafiki yangu, acha Roho Mtakatifu akudhihirishie mshangao na uzuri wa upendo wa Mungu kwako kupitia Neno lake.  Yeye amechunguza mafumbo ya Mungu ili akudhihirishie haya: kwamba huwezi kuanza kufikiria mema yote aliyoyaandaa kwa ajili yako.  Chukua muda wa kutosha kuyatafakari hayo.  

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.