... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

kuongozwa na roho

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Yohana 10:4,5 Naye awatoapo nje kondoo wake wote, huwatangulia; na wale kondoo humfuata, kwa maana waijua sauti yake. Mgeni hawatamfuata kabisa, bali watamkimbia; kwa maana hawazijui sauti za wageni.

Listen to the radio broadcast of

kuongozwa na roho


Download audio file

Kuruhusu mtu mwingine kukuongoza, kwa wengi katika dunia hii ya leo, ni kero kabisa.  Jamani!  Nataka kufanya kama ninavyopenda mimi.  Sitaki kufuata mtu mwingine.  Wewe je!?

Mimi, kama mtu aliyewahi kuwa jeshini, naweza kukwambia kwamba hakuna kitu kingine kinachoweza kuridhisha kama vile, kutembea kama askari kwenye uwanja wa gwaride halafu baada ya kumaliza na kutoka uwanjani, ukijua kwamba wewe pamoja na wanajeshi wenzako mmetimiza vizuri sana zoezi kwa usahihi kabisa bila kukosa.

Wakati wa baridi, tulivaa sare za blu nyeusi na glovu nyeupe.  Jamani!  Fikiria  mwako wa glovu 450 nyeupe tulipendeza kabisa.  Tulipendesa na huku tukiwa tumevalia buti nyeusi.

Ebu fikiria ingekuwa vurugu gani kama katika zoezi, kila mwanajeshi angeamua kufanya anavyotaka yeye; kama angepuuza amri za viongozi?  Siku moja Yesu alisema hivi:

Yohana 10:4,5  Naye awatoapo nje kondoo wake wote, huwatangulia; na wale kondoo humfuata, kwa maana waijua sauti yake.  Mgeni hawatamfuata kabisa, bali watamkimbia; kwa maana hawazijui sauti za wageni.

Kwa nini Wakristo wengi wanazurua maishani wakiwa na mtazamo wa kutojali viongozi wao, wakizurua kote kote?

Sikiliza sauti yake Yesu, umtii, umfuate. 

Na Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.


We use cookies to improve your browsing experience, analyse site traffic & personalise content, but we do not track you when you leave this site. To find out how we utilise & protect your data, check out our "Privacy Policy".

Privacy Policy