... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Siku ya Kuadhimisha Mapatano ya Kusimamisha Vita

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

1 Wakorintho 15:20-22 Lakini sasa Kristo amefufuka katika wafu, limbuko lao waliolala. Maana kwa kuwa mauti ililetwa na mtu kadhalika na kiyama ya wafu ililetwa na mtu. Kwa kuwa kama katika Adamu wote wanakufa, kadhalika na katika Kristo wote watahuishwa.

Listen to the radio broadcast of

Siku ya Kuadhimisha Mapatano ya Kusimamisha Vita


Download audio file

Hivi karibuni tumechunguza swala la ufufuko wa Yesu.  Na kama alifufuka kweli kweli, ina maana gani kwetu?, na kama ilitokea kweli, ina maana gani kwako na kwangu katika maisha ya sasa na kuendelea hadi milele?

Ni swali nyeti, ni vizuri kuongea yaliyotokea zamani – tena ni sahahi kupata uhakika wa mambo katika fikra zetu ili imani yetu ijengwe kwenye msingi imara – lakini kufufuka kwa Yesu kutaleta mabadiliko gani kiutendaji katika mienendo yetu ya sasa na hata milele? 

Leo ni siku ya kuadhimisha Mapatano ya Kusimamisha Vita, Vita ile ya Kwanza ya Dunia Nzima iliyosimamishwa miaka 104 iliyopita.  Watu ma-milioni walikufa.  Milio ya bunduki haikusikika tena, lakini baada ya mapatano yale, watu walijiuliza, itakuwaje sasa?  Walioumizwa na ukatili wa vita walitakiwa kusahau yaliyopita na kutazamia ya mbele. 

Hata sisi, wewe na mimi, inatubidi tutazamie yaliyo mbele kwasababu siku moja, maiti zetu zitalala kwenye jeneza zikiwekwa tayari kwa ajili ya maziko. mauti haiepukiki, Hatima yako itakuwaje? 

1 Wakorintho 15:20-22  Lakini sasa Kristo amefufuka katika wafu, limbuko lao waliolala.  Maana kwa kuwa mauti ililetwa na mtu kadhalika na kiyama ya wafu ililetwa na mtu.  Kwa kuwa kama katika Adamu wote wanakufa, kadhalika na katika Kristo wote watahuishwa. 

Dhambi zetu ni kama tangazo la vita dhidi ya Mungu.  Lakini kupitia msalaba wa Kristo, yeye kwa upande wake, alitangaza mapatano ya kusimamisha vita, alitangaza amani.  Sasa kupitia kaburi lile ambalo liko wazi, Mungu alitangaza pia hatima nzuri endelevu, maisha mapya, uzima unaotokana na ufufuo kwa wale wote wanaomwamini Mwanaye Yesu. 

Dakika ile ile tunapoweka imani yetu kwa Yesu, tunahuishwa tangu sasa hadi milele.  

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.


We use cookies to improve your browsing experience, analyse site traffic & personalise content, but we do not track you when you leave this site. To find out how we utilise & protect your data, check out our "Privacy Policy".

Privacy Policy