... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Kupita Mawazo Yetu

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

1 Korintho 2:9,12 Lakini, kama ilivyoandikwa, Mambo ambayo jicho halikuyaona wala sikio halikuyasikia, (wala hayakuingia katika moyo wa mwanadamu,) mambo ambayo Mungu aliwaandalia wampendao. ... Lakini sisi hatukuipokea roho ya dunia, bali Roho atokaye kwa Mungu, makusudi tupate kuyajua tuliyokirimiwa na Mungu.

Listen to the radio broadcast of

Kupita Mawazo Yetu


Download audio file

Je!, Kuna wakati unajikuta unazunguka-zunguka tu huku ukibanwa na pirika-pirika za maisha?  Halafu hatimaye mizunguko hiyo inakupelekea kupoteza furaha uliyokuwa nayo.

Fiziksi ni ya ajabu sana, yaani sponji haiwezi kukausha maji ikiwa kavu, ni lazima uichovye kwenye maji kwanza ndipo iweze kufuta maji, ahahaha, ni ajabu.

Sijui kama umeshafanya huo utafiti, yawezekana leo unahitaji kuzamishwa kwenye maji na kukamuliwa ili furaha ile isiyoneneka irudishwe ndani ya moyo wako.  Basi tuanzie kwa kutumia mstari huu:

1 Korintho 2:9  Lakini, kama ilivyoandikwa, Mambo ambayo jicho halikuyaona wala sikio halikuyasikia, (wala hayakuingia katika moyo wa mwanadamu,) mambo ambayo Mungu aliwaandalia wampendao.   

Halafu Mtume Paulo anaongeza kwa kusema kwamba, hata watawala wakubwa wa dunia hii hawakuelewa.  Ndiyo maana walimsulubisha Yesu.  Lakini … 

1 Korintho 2:12  Lakini sisi hatukuipokea roho ya dunia, bali Roho atokaye kwa Mungu, makusudi tupate kuyajua tuliyokirimiwa na Mungu. 

Na katika Kristo, tayari Mungu ameshaandaa mibaraka ya ajabu-ajabu kwa ajili yako … tangu leo na hata milele, acha Roho Mtakatifu akuzamishe leo, na uliruhusu Neno la Mungu likukamue.

Kwasababu mambo mema alikuandalia kwa ajili yako – hata kama mazingira yako hayapendezi – mambo yale yanapita mawazo yetu kabisa.  

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.


We use cookies to improve your browsing experience, analyse site traffic & personalise content, but we do not track you when you leave this site. To find out how we utilise & protect your data, check out our "Privacy Policy".

Privacy Policy