... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Kazi ya Mkulima

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

1 Korintho 3:6,7 Mimi nilipanda, Apolo akatia maji; bali mwenye kukuza ni Mungu. Hivyo, apandaye si kitu, wala atiaye maji, bali Mungu akuzayo.

Listen to the radio broadcast of

Kazi ya Mkulima


Download audio file

Mtu anapomfanyia Mungu kazi nzuri akitumia vipaji vyake,  vipawa vyake, muda wake pamoja na rasilimali zake ili aweze kushirikisha wengine upendo wa Kristo, kusema ukweli, mara nyingi huwa kuna mtego  wa kuwa na kiburi.

Zamani nilikuwa kwenye huduma ambayo kiongozi wetu – mtu aliyefaulu sana kwenye huduma yake – alianza kujiamini kupita kiasi.  Alijiona kama “mtu maarufu”. 

Hatimaye alianza kudhulumu watu, kuwafarakisha na kuwatenga.  Mimi nilikuwa mmojawapo wa waliotengwa, iliniumiza sana.  Kwa miaka ishirini nikiwa kwenye huduma, nimetoa machozi mara mbili tu.  Wakati ule nilipotengwa.  Lakini mwishowe, baada ya miaka mingi bodi ya hudumu ilimfukuza yule kiongozi kwasababu mambo yalikuwa yameshaharibika sana. 

Unajua, mimi nina uhakika kwamba mtu anapoanza kunia makuu na kuona kwamba yeye ni topu kabisa na kuwa na kiburi … Mungu huwa hana haja naye tena.  Mtume Paulo alisema hivi miaka mingi iliyopita: 

1 Korintho 3:6,7  Mimi nilipanda, Apolo akatia maji; bali mwenye kukuza ni Mungu.  Hivyo, apandaye si kitu, wala atiaye maji, bali Mungu akuzayo. 

Unajua, inabidi tujikague leo –Je!  Tumeanza kuamini propaganda zetu sisi wenyewe?, Je!  Tumeanza kunia makuu kuliko inavyotupasa kunia? 

Kwasababu kazi ya mkulima (yaani wewe na mimi) ni kupanda na kumwagilizia tu.  Lakini Mungu ndiye akuzaye. 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.