... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Kupokea Ushauri wa Mtu Aliyefungwa Jela

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Waefeso 4:2 Kwa unyenyekevu wote na upole, kwa uvumilivu, mkichukuliana katika upendo.

Listen to the radio broadcast of

Kupokea Ushauri wa Mtu Aliyefungwa Jela


Download audio file

Kama mtu angekuandikia barua kutoka gerezani akikushauri jinsi inavyokupasa kuishi, je!  Ungepokea ushauri wake?  Naona ingetegemeana lakini bila shaka ungalikuwa na mashaka, si kweli?

Wafungwa wengi wanadai kwamba wameonewa, kwamba hawana hatia.  Isitoshe kuna hatari gerezani inayotokana na wafungwa wengine, na mtazamo hasi mtu akizingatia jinsi miezi na miaka inavyoenda, kwa kweli hali hiyo haina budi kuchanganya mawazo yao.  Kwa hiyo, ushauri wo wote ambao wangetoa kwa wengine, pengine usingekuwa ushauri bora.

Mtume Paulo alikaa gerezani muda wa kutosha, akisubiria hukumu ya kifo.  Yeye, kwa kweli, alifungwa kinyume cha haki, kwa sababu alikuwa anatangaza habari njema ya Yesu tu.

Lakini hakuwahi kunung’unika kwa sababu alifungwa mnyororo kwa walinzi wake, wala hakulalamikia mazingira yale mabaya na uonevu.  Badala yake, aliandika nyaraka zilizojaa hekima ya kama ifuatavyo…

Waefeso 4:2  Kwa unyenyekevu wote na upole, kwa uvumilivu, mkichukuliana katika upendo.

Ebu fikiria jinsi mtu ambaye aliyekuwa katika mazingira yale kuandika maneno kama hayo?  Bila shaka, Roho Mtakatifu alikuwa anafanya kazi kwa nguvu moyoni mwake, si kweli?  

Na wewe, rafiki yangu, wakati unajisikia kwamba umeonewa, wakati tu mahali pagumu, wakati watu wengine wanatuumiza – kuufuata ushauri wa Paulo kutoka gerezani kunahitaji nguvu za Roho Mtakatifu pia.

Roho mtakatifu ni jawabu la kila kitu.

Kwa unyenyekevu wote na upole, kwa uvumilivu, mkichukuliana katika upendo.

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.


We use cookies to improve your browsing experience, analyse site traffic & personalise content, but we do not track you when you leave this site. To find out how we utilise & protect your data, check out our "Privacy Policy".

Privacy Policy