Kuridhika Nafsini Mwako
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Zaburi 63:5-8 Nafsi yangu itakinai kama kushiba mafuta na vinono; kinywa changu kitakusifu kwa midomo ya furaha. Ninapokukumbuka kitandani mwangu, nakutafakari Wewe makesha yote ya usiku. Maana Wewe umekuwa msaada wangu, na uvulini mwa mbawa zako nitashangilia. Nafsi yangu inakuandama sana; mkono wako wa kuume unanitegemeza.
Kuridhika. Kutoshelezeka. Kutimiziwa. Maneno hayo matatu yanaeleza habari ya ustawi ambao kila mmoja wetu anautafuta kwa hamu kubwa … lakini wengi hawaufikie kabisa.
Tafadhali uniwie radhi kwanza, kwa sababu leo ninaadhimisha miaka 65 tangu nilipozaliwa hapa duniani tarehe 15 ya Machi 1959. Ni ajabu, nimetimiza miaka 65! Ina maana inanifanya kuwa mimi ninazidi umri asilimia 90% ya watu wanaoishi ulimwenguni leo.
Pia, ina maana kwamba nimekuwa na uzoefu usio mdogo. Macho haya yameona mengi na sasa nimekuwa na imvi, nimetafakari mengi na moyo wangu umefurahia mengi na kuhuzunikia mengi.
Kwa hiyo, nikiwa na umri huu na uzowefu huu, naweza kukuhakikishia kwamba mali, mafanikio, na kujulikana sana katika fani yake haviwezi kumridhisha mtu, haviwezi kumtosheleza wala kumtimizia haja ya moyo wake. Kuna Mmoja tu awezaye kuridhisha kabisa:
Zaburi 63:5-8 Nafsi yangu itakinai kama kushiba mafuta na vinono; kinywa changu kitakusifu kwa midomo ya furaha. Ninapokukumbuka kitandani mwangu, nakutafakari Wewe makesha yote ya usiku. Maana Wewe umekuwa msaada wangu, na uvulini mwa mbawa zako nitashangilia. Nafsi yangu inakuandama sana; mkono wako wa kuume unanitegemeza.
Maneno hayo yaliandikwa na Mfalme Daudi akiwa jangwani mwa Uyahudi. Sehemu ngumu sana. Sehemu inayoonekana kuwa mbali na Mungu. Lakini ndipo moyo wake uliposhibishwa kama kwenye karama yenye mafuta na vinono.
Kuridhika. Kutoshelezeka. Kutimiziwa. Kunapatikana sehemu moja tu. Kwa Mungu Mwenyewe.
Nafsi yangu inakuandama sana; mkono wako wa kuume unanitegemeza.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.