Kushinda Ulimwengu
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Zaburi 37:34-36 Wewe umngoje BWANA, Uishike njia yake, naye atakutukuza uirithi nchi, wasio haki watakapoharibiwa utawaona. Nimemwona mtu aisye haki mkali sana akijieneza kama mwerezi wa Lebanoni. Nikapita na kumbe! Hayuko, nikamtafuta wala hakuonekana.
Hakuna uhaba wa waovu duniani, waovu bado wapo wengi sana. Ndio maana, usishangae kukutana nao kila mara.
Mfalme Daudi anajulikana kama mfalme mkubwa kupita wafalme wote wa Israeli, hadi pale Mfalme aitwaye Yesu – alipozaliwa miaka elfu baada ya utawala wa Daudi.
Ninachopendelea sana kuhusu mtu huyu, nikakithamini pia, ni namna Daudi alivyoweza kuandika mengi, maneno tunayokuta katika kitabu cha Zaburi ndani ya Agano la Kale. Karibu Zaburi zote zilikuwa ni nyimbo zilizoimbwa na wana wa Israeli kama sehemu ya kumwabudu Mungu.
Ndio maana tunaweza kusema kwamba Zaburi zimejaa sifa na maabudu, na kwasababu Daudi aliishi maisha magumu mno, kuna zaburi za maombolezo nyingi kuliko za sifa. Shida alizokutana nazo Daudi, zilitokana na waovu wengi aliokutana nao katika maisha yake.
Ndio maana neno hili la hekima ni la maana sana:
Zaburi 37:34-36 Wewe umngoje BWANA, Uishike njia yake, naye atakutukuza uirithi nchi, wasio haki watakapoharibiwa utawaona. Nimemwona mtu aisye haki mkali sana akijieneza kama mwerezi Usiwa Lebanoni. Nikapita na kumbe! Hayuko, nikamtafuta wala hakuonekana.
Ni jambo la hekima la maana kabisa, Usiruhusu waovu unaokutana nao wakusumbue, hata kama wanaonekana kuwa na nguvu. Endelea tu kufanya yale ambayo Bwana akwambia uyafanye ukingoja msaada wake. Usiwe na mashaka. Mungu atakabiliana nayo.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.