Kutafutwa Sana
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Mariko 1:35-37 Hata alfajiri na mapema sana akaondoka, akatoka akaenda zake mahali pasipokuwa na watu, akaomba huko. Simoni na wenziwe wakamfuata; nao walipomwona wakamwambia, Watu wote wanakutafuta.
Ni rahisi mtu kujidanganya kwa kufikiri kwamba; yeye ni mtu muhimu duniani kuliko wengine; kwamba huduma zake zinatafutwa sana; yuko busy, busy, busy, na ndio lengo la maisha yake.
Ni wazi kwamba; sote tunapitia vipindi ambavyo hatuwezi kuvikwepa; muda tulio nao hautoshi kutimiza majukumu yetu yote, Mzazi yoyote anayelea watoto atakuthibitishia hayo nisemayo. Hata mtu anayefanya vibarua vitatu kwa waajiri tofautitofauti, naye pia atayathibitisha hayo.
Lakini hali hiyo ni kama hatua fulani tu, hatimaye; mtu anaweza kuzipita, si kwamba ni hali endelevu!.
Haijalishi unabanwaje na ratiba yako, ninataka kuweka tahadhari kwamba, usijidanganye; kwamba huna muda tena wa maombi (na hii ndio udhuru ya kwanza, wengi wanaitumia kujitetea pale maombi yao yanaposua-sua.
Nadhani hakuna mwingine aliyetafutwa sana kama Yesu. Alikuwa amejulikana sana, maarufu kabisa. Mji mzima uliweza kutoka kwenda kumkuta kwenye mbuga. Maisha yake ndivyo ilivyokuwa.
Mariko 1:35-37 Hata alfajiri na mapema sana akaondoka, akatoka akaenda zake mahali pasipokuwa na watu, akaomba huko. Simoni na wenziwe wakamfuata; nao walipomwona wakamwambia, Watu wote wanakutafuta.
Hata kama alikuwa anatafutwa sana, daima; Yesu alitafuta muda wa kuomba. Ni kwasababu ndipo panapotokea uwezo, amani na hekima. Hakikisha umetenga muda wa maombi.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.