Kutathmini Yaliyopita
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
2 Wakorintho 7:10 Maana huzuni iliyo kwa jinsi ya Mungu hufanya toba liletalo wokovu lisilo na majuto; bali huzuni iliyo kwa jinsi ya Mungu hufanya toba liletalo wokovu lisilo na majuto; bali huzuni ya dunia hufanya mauti.
Baada ya siku chache tuaanza mwaka mpya. Kwa kweli, ni siku nyingine tu, ila dhana ya mwaka mzima kupita inasababisha mtu kutafakari.
Siku hizi chache zilizopita, tumejikuta mara nyingi tunatathmini mwaka huu unaoenda kwisha – vipindi vizuri na vibaya, ushindi na hasara, maamuzi yetu yenye busara na makosa tunayoyajutia.
Kwa nini tunafanya hivyo? Ni kwa sababu inatusaida tuweze kuweka kando yaliyopita. Tusipoyaweka kando, yale mabaya, hasara zile na makosa yale yataendelea kututikisa.
Kwa hiyo, ukitathmini mwaka huu unaokaribia kwisha, acha nikupe Neno litokalo kwa Mungu linaloweza kukusaidia kuweka kando huzuni zile zote zinazotakiwa kufutwa:
2 Wakorintho 7:10 Maana huzuni iliyo kwa jinsi ya Mungu hufanya toba liletalo wokovu lisilo na majuto; bali huzuni iliyo kwa jinsi ya Mungu hufanya toba liletalo wokovu lisilo na majuto; bali huzuni ya dunia hufanya mauti.
Huzuni ni kama upanga ukatao kuwili. Inaweza kuwa jambo jema au baya. Inaweza kutusukuma kubadilisha mwenendo wetu na kujirekebisha; au inaweza kusababisha tugaagae katika mtazamo hasi . Sikiliza vizuri ukitathmini mwaka wako, ukianza kuuweka kando:
Huzuni iliyo kwa jinsi ya Mungu hufanya toba liletalo wokovu lisilo na majuto.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.