Kuthamini Jitihada za Watu Wengine
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Wafilipi 2:3,4 Msitende neno lo lote kwa kushindana wala kwa majivuno; bali kwa unyenyekevu, kila mtu na amhesabu mwenziwe kuwa bora kuliko nafsi yake. Kila mtu asiangalie mambo yake mwenyewe, bali kila mtu aangalie mambo ya wengine.
Hivi, Umewahi kujitahidi kutumika kwa nguvu zako zote lakini watu hawathamini yale unayowatendea? Huwa unajisikia kama hufai, sindiyo?, na kwa kusema ukweli, ni lazima mtu ujisikie uchungu moyoni.
Siku zilizopita hapa kwetu kwenye studio zetu za Christianityworks ( yaani Ukristo Unafanya Kazi), tulikuwa tunaandaa kipindi kinachotangazwa kote ulimwenguni lakini pia kilitengenezwa hasa kwa manufaa ya kituo fulani cha redio kwenye nchi fulani ambayo sitaitaja ili kiweze kwenda sambamba na mfumo wao wa lugha na sauti, ilitugharimu pesa nyingi kufanya hivyo.
Lakini, siku moja tuligundua kwamba, wao walikuwa wameacha kutangaza kipindi chetu kwa muda wa miezi 18 bila kututaarifu, kweli, nadhani utanielewa kama nitakwambia kuwa ilituhuzunisha sana … si kwamba waliacha kutangaza kipindi hicho tu, bali walitupuuza kiasi cha kuto kutupatia taarifa wakati sisi tulikuwa tunawatengezea vipindi maalum kwa ajili yao tu tena kwa gharama.
Wafilipi 2:3,4 Msitende neno lo lote kwa kushindana wala kwa majivuno; bali kwa unyenyekevu, kila mtu na amhesabu mwenziwe kuwa bora kuliko nafsi yake. Kila mtu asiangalie mambo yake mwenyewe, bali kila mtu aangalie mambo ya wengine.
Nataka nieleweke vizuri, Watu walioko kwenye kituo kile cha redio si watu wabaya, hapana!, ni watu wazuri kabisa lakini sema tu sehemu ya kwanza ya vipindi vile haiwahusu kabisa hata kidogo! Unaona, nirahisi sana mtu kupuuza mtu mwingine bila ya kukusudia, na kwa vile tuko bize sana nirahisi mtu kufikiri kwamba hathaminiwi hata kidogo.
Sidhani kama unataka kuonekana kama humthamini mtu, hata mimi sipendi kuonekana hivyo. Lakini, hata hivy ninafahamu kwamba hata kile kituo cha redio hakikukusudia kuonekana kwamba kimepuuza japo ndivyo walivyotafsirika.
Kila mtu asiangalie mambo yake mwenyewe, bali kila mtu aangalie mambo ya wengine. Usisahau kujali watu.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.