... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Kuishi Tofauti

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Yohana 13:34,35 Amri mpya nawapa, Mpendane. Kama vile nilivyowapenda ninyi, nanyi mpendane vivyo hivyo. Hivyo watu wote watatambua ya kuwa ninyi mmekuwa wanafunzi wangu, mkiwa na upendo ninyi kwa ninyi.

Listen to the radio broadcast of

Kuishi Tofauti


Download audio file

 Jana tulijadili habari ya mtu kujitanguliza, kwasababu mara nyingi HUWA tunajali mambo yetu tu na kupuuza mahitaji ya watu wengine. Sasa tunawezaje kuishi tofauti?

Sijui kama umewahi kuhisi kama mambo yote ya ki-Mungu yaliyomo kwenye Biblia, kwamba hayana uhusiano na hali halisi ya maisha ya kila siku katika karne yetu hii ya 21!?.  

Lakini mawazo hayo si kweli!, Hususani mtu anapoishi maisha ya kusaidia wengine na kuwatanguliza badala ya kujitanguliza yeye mwenyewe, ndivyo Yesu alivyolenga pale aliposema maneno yafuatayo:

Yohana 13:34,35  Amri mpya nawapa, Mpendane. Kama vile nilivyowapenda ninyi, nanyi mpendane vivyo hivyo.  Hivyo watu wote watatambua ya kuwa ninyi mmekuwa wanafunzi wangu, mkiwa na upendo ninyi kwa ninyi. 

Labda umeishasikia maneno haya mara nyingi, kwahiyo ni rahisi kuyapokea kwa juu-juu.  Lakini tutafakari kwanza … hivi, Maisha yetu iyangekuwaje kama tungeishi kulingana na  maneno ya Yesu?  Inaonekana kwamba, inawezekana mtu akaishi bila anasa!?,  inawezekana mtu akaishi maisha ya upendo na ukarimu huku akiwajali wengine kabisa na kuongea nao kwa upole na huruma. 

Ndivyo anavyoongea Yesu hapa, hivi, tungeleta mabadiliko gani kwenye maisha ya watu wengine kama tungeishi kwa upendo kazini, nyumbani na hata katika matumizi ya pesa tulizo nazo?

Ishi pasipo anasa, kama kawaida tu, Upende kwa ukarimu, Uwajali watu wengine kwelikweli na uongee na watu kwa huruma. 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.