Kutii Sheria ya Kristo
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Wagalatia 6:2 Mchukuliane mizigo na kuitimiza hivyo sheria ya Kristo.
Ebu tuseme kwamba moyoni mwako kwa kweli kuna shauku ya kutenda jambo jema; unataka kufanya yale Mungu anayokuagiza ufanye. Lakini kama tulivyoona jana, mara nyingi ni vigumu … si kweli?
Si rahisi! Kuna siku ni kama haiwezikani kabisa. Ndio hali halisi ya mambo. Unatoka nyumbani asubuhi kila siku ukiwa na nia njema, lakini unakutana na mtu fulani au tukio fulani na unakwazika tena pale pale kama ulivyofanya jana, na juzi na siku zilizopita.
Lakini Mungu, nilitaka kutenda mema … lakini yule mkorofi alikuja na kunichokoza, kwa hiyo nilimfokea kabisa.
Ndivyo inavyoenda. Huwa inatutokea sisi sote kutoka kwenye mazingira tofauti-tofauti. Kwahiyo, leo hii, inabidi tupige hatua nzuri, tuwe na kipaumbele kwa kufanya lililo jema.
Wagalatia 6:2 Mchukuliane mizigo na kuitimiza hivyo sheria ya Kristo.
Kwa kweli ni Andiko lenye nguvu. Wakorofi wale wanaotusumbua, kumbe na wao wana matatizo, wamebanwa na shida zao, wanaumia, wengine wanateswa na pepo wachafu. Mara nyingi hatuelewi wanavyosumbuka. Mimi ninaamini na nina uhakika kwamba leo, kupitia Neno la Mungu atatupa uwezo wa kuwatendea tofauti. Badala ya kuwachukia, tunaweza kuwasaidia wakati wa shida.
Ebu tulia na kutafakari hayo kwa muda wa kutosha. Tukiamua kuwapenda badala ya kuwafokea, kumbe tutakuwa tunaitimiza sheria ya Kristo.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.