... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Kuwa Mtu Yule Ambaye Mungu Anataka Uwe

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Wakolosai 1:28 Ambaye sisi tunamhubiri habari zake tukimwonya kila mtu, na kumfundisha kila mtu katika hekima yote, tupate kumleta kila mtu mtimilifu katika Kristo.

Listen to the radio broadcast of

Kuwa Mtu Yule Ambaye Mungu Anataka Uwe


Download audio file

Maisha ni mapambano, si kweli?  Kila wakati, siku baada ya siku kuna changamoto, kuna migongano, wasiwasi … n.k.  Nadhani unanielewa.  Kwa hiyo acha nikuulize, je! Umeandaliwa vya kutosha ili ukabiliane na hayo yote?

Kikawaida inatakiwa  tukue kila siku, hadi tufikie uwezo wa kukabiliana na changamoto kuzidi miaka mitano iliyopita, kwa mfano, kama ukijilinganisha jinsi ulivyo leo na jinsi ulivyokuwa miaka mitano iliyopita, je!, umekua?  Je!  Umekomaa?  Unao uwezo wa kupambana vizuri kuliko wakati ule? 

Kama jibu lako ni ndio, basi hongera. Lakini kama ni hapana, lazima ujiulize … ni kwanini?  Unajua, Mungu ana mpango kwa ajili yako ili ukue – si katika nguvu na maazimio tu, si katika hekima tu (hata kama ni muhimu sana) lakini pia, ukue katika unyenyekevu na neema … ili ubadilike kuwa mtu yule anayetaka uwe.  Sikiliza: 

Wakolosai 1:28  Ambaye sisi tunamhubiri habari zake tukimwonya kila mtu, na kumfundisha kila mtu katika hekima yote, tupate kumleta kila mtu mtimilifu katika Kristo. 

Maono ya Mungu kwako ni kwamba, anatka ukue hadi uwe mtu mkamilifu ndani ya Kristo.  Je! Ndiyo maono yako pia?  Na kama ni kweli, je! Unafanyaje ili uyatimize?  Je!, Unapokea hekima yake, ushauri wake, mafundisho yake na Neno lake?  Je!  Unayaishia? 

Kuna mtu fulani aliwahi kutoa wazo kwamba, ili mtu aweze kwenda sambamba na maono ya Mungu, aanze kuandika maneno ambayo watu wengetumia kumsifu wakati wa mazishi yake, halafu aendelee kuyasahihisha mara kwa mara kwa sababu lengo la Mungu ni kwamba uweze kuendelea kukua na kukomaa kiroho ndani ya Kristo.  

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.


We use cookies to improve your browsing experience, analyse site traffic & personalise content, but we do not track you when you leave this site. To find out how we utilise & protect your data, check out our "Privacy Policy".

Privacy Policy