... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Kwa Ajili ya Mmoja Tu

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Wagalatia 1:10 Maana, sasa je! Ni wanadamu ninaowashawishi, au Mungu? Au nataka kuwapendeza wanadamu? Kama ningekuwa hata sasa nawapendeza wanadamu, singekuwa mtumwa wa Kristo.

Listen to the radio broadcast of

Kwa Ajili ya Mmoja Tu


Download audio file

Inakaribia miaka thelathini sasa tangu baba yangu mpendwa aage dunia. Bado namkumbuka. Bado natamani angekuwepo ili tuongee.  Si alikuwa baba mzazi?  Lakini najiuliza, hivi, kuna watu wengine duniani wanamkumbuka baba!?.

Nadhani si wengi wanamkumbuka, Wale wote aliokuwa anafanya nao kazi kwenye kiwanda cha vyuma; wanakwaya aliokuwa anawaongoza kwenye kwaya yao, hivi Wanamkumbuka kweli?  Ni kweli, hata badhi ya wenzake wameshakufa lakini nadhani kwamba,  tofauti na mama yangu na mimi, hakuna mtu mwingine duniani anayewaza habari za baba yangu, hata kama alikuwa mtu mwema kabisa.  Sasa ntaka kusema nini hapo!? 

John Chrysostom mnamo mwaka 387 baada ya Kristo alisema hivi – “Kama ungefahamu namna watu watakavyokusahau haraka baada kufa, usingetafuta kumpendeza mtu yoyote ila Mungu tu.” 

Ni kweli, lazima tuwatendee wengine mema. Lakini tukiyatenda kwa lengo la kuwashawishi au kupongezwa, itakuwa thawabu ya muda mfupi.  Mtume Paulo alisema hivi: 

Wagalatia 1:10  Maana, sasa je!  Ni wanadamu ninaowashawishi, au Mungu?  Au nataka kuwapendeza wanadamu?  Kama ningekuwa hata sasa nawapendeza wanadamu, singekuwa mtumwa wa Kristo. 

Ina maana, katika yote aliyoyafanya duniani, hata yale mema aliyowatendea wengine – ikiwemo wewe na mimi ambao bado tunafaidika nayo – kweli alikuwa anayafanya yote machoni pa mtu mmoja tu.  Alikuwa anayafanya kwa ajili ya Mungu peke yake. 

Kupendeza binadamu ni kazi bure, ni kufuatilia wenye kigeugeu tu. Siku moja wanakupongeza, kesho yake wanapiga kelele na kusema “asulubiwe!” si kweli?  Kwa vyo vyote, endelea kutenda mema, lakini yatende kwa ajili ya Mungu.  

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.


We use cookies to improve your browsing experience, analyse site traffic & personalise content, but we do not track you when you leave this site. To find out how we utilise & protect your data, check out our "Privacy Policy".

Privacy Policy