Kwa Hiyo, Usiogope
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Isaya 41:9,10 Wewe u mtumishi wangu; nimekuchagua wala sikukutupa; usiogope, kwa maana mimi ni pamoja nawe; usifadhaike, kwa maana mimi ni Mungu wako; nitakutia nguvu, naam, nitakusaidia, naam, nitakushika kwa mkono wa kuume wa haki yangu.
Je! Unamwamini Yesu? Kama unamwamini Yesu, basi imani yako ndani yake imekusudiwa kukupa ushindi. Ushindi dhidi ya dhambi yako na ushindi juu ya mazingira yako. Kwa sababu mara nyingi, hayo mawili kwa pamoja yanatisha mno.
Kama wewe mwenyewe umejichimbia shimo kwasababu umemwasi Mungu halafu mawingu ya dhoruba yanakuja, kuna radi na ngurumo … kweli panatisha mno! Na inazidi kutisha sana kwa sababu kwa sehemu angalau, unafahamu kwamba ni kosa lako.
Lakini maisha ndivyo yalivyo, maisha ya mtu ambaye hajakamilika kama wewe au mimi, Na kama tunataka kuendelea kuongea habari za kukuza imani zetu – na ndiyo mada yetu wiki hii kwenye kipindi chetu cha Neno Safi Lenye na Afya – lazima tushuke pamoja kwanza ndani ya shimo lile linalotisha lenye giza … na kumruhusu Mungu aangaze nuru yake mahali pale.
Isaya 41:9,10 Wewe u mtumishi wangu; nimekuchagua wala sikukutupa; usiogope, kwa maana mimi ni pamoja nawe; usifadhaike, kwa maana mimi ni Mungu wako; nitakutia nguvu, naam, nitakusaidia, naam, nitakushika kwa mkono wa kuume wa haki yangu.
Dua yangu kwa ajili yako ni kwamba upokee Neno lenye nguvu kutoka kwake, kujua bila shaka hata kidogo kwamba ukweli huu ni hakika hususani mle kwenye shimo lile la giza.
Kwa sababu hapo ndipo neema ya Mungu pamoja na rehema zake zinaweza kukuonekania kwa wingi zaidi. Usikatishwe tamaa hata siku moja. Usikose hata siku moja kutazama upendo wa Kristo wa namna nyingi tofauti tofauti. Kwasababu kwenye shimo lile ni sehemu ambapo mtu anahonja utamu wake mwenyewe kuliko mahali pengine popote.
Mungu amekusudia kuimarisha imani yako kwake, mle ndani ya shimo.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.