... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Kwa Tahadhari

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Mwanzo 2:23,25 Kwa hiyo mwanamume atamwacha baba yake na mama yake naye ataambatana na mkewe, nao watakuwa mwili mmoja. Nao walikuwa uchi wote wawili, Adamu na mkewe, wala hawakuona haya.

Listen to the radio broadcast of

Kwa Tahadhari


Download audio file

Kuishi kwenye si rahisi siku zingine. Kuna mambo mengi yanakusanyikia juu ya ndoa ili ivunjike – mfano, ule uongo unaosema kwamba kupeana talaka ni kawaida, ni hiari ya mtu, kuna magonjwa, majonzi hata kufiwa na mtoto.

Kuna takimwu inayohuzunisha mno, ni kwamba, wanandoa waliofiwa na mtoto wana uwezekano wa kuachana kuliko wale ambao hawajafiwa na mtoto.  Baada ya kupotelewa na mtoto, ndipo mume na mke wanakuwa na haja ya upendo wa mwenzi kuliko nyakati zingine. 

Halafu kwa upande mwingine, kuna baadhi ya watu huwa wanaamka na kuamua kwamba hawana upendo tena na mume wake au mke wake.  Nilisoma habari iliyoandikwa na mwanamke fulani akipelekwa na mume wake kwenye mgahawa, wakiwa wanakula, mume aliweka hati ya talaka mezani kubatilisha ndoa yao. 

Ina maana kwamba, kuna wanandoa wasiokuwa na sababu za kupeana talaka. Kwa nini wasiachane?!  Acha nikwambie ni kwa nini hawawezi kusubutu. 

Mwanzo 2:23,25  Kwa hiyo mwanamume atamwacha baba yake na mama yake naye ataambatana na mkewe, nao watakuwa mwili mmoja.  Nao walikuwa uchi wote wawili, Adamu na mkewe, wala hawakuona haya. 

Kule kumepoandikwa “kuambatana” maana yake ni kuunganika daima.  Watakuwa mwili mmoja. Yaani ni uhusiano wa undani kabisa.  Nao walikuwa uchi wote wawili, Adamu na mkewe, wala hawakuona haya. 

Wakati Mungu anaunganisha watu wawili hivyo, kuwatenganisha ni kitanzi kinachoumiza mno kuliko vyote.  Haikukusudiwa iwe hivyo.  Labda kuwe na ukatili na ubabe au tabia ya kuzini, hapo mmoja atalazimika kutafuta nyaraka za talaka. Lakini tofauti na hapo, kama umewahi kuwaza kumfukuza mwenzi wako, acha kabisa.  Wawili wameshakuwa mwili mmoja.  

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.


We use cookies to improve your browsing experience, analyse site traffic & personalise content, but we do not track you when you leave this site. To find out how we utilise & protect your data, check out our "Privacy Policy".

Privacy Policy