Lengo Kuu la Upendo wa Mungu
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
1 Yohana 4:10-12 Hili ndilo pendo, si kwamba sisi tulimpenda Mungu, bali kwamba yeye alitupenda sisi, akamtuma Mwanawe kuwa kipatanisho kwa dhambi zetu. Wapenzi ikiwa Mungu alitupenda sisi hivi, imetupasa na sisi kupendana. Hakuna mtu aliyemwona Mungu wakati wo wote. Tukipendana, Mungu hukaa ndani yetu, na pendo lake limekamilika ndani yetu.
Ninakuomba, thafadhali, jaribu kufikiria mtu anayekusumbua kuliko wote. Bado ukimtafakari, jaribu pia kukumbuka jinsi mlivyohusiana hivi karibuni. Kumfikiria hivyo imekugusaje?
Nimechagua anayesumbua kuliko wote ili niweze kusisitiza kweli kwamba sio rahisi kupenda watu ambao hawajakamilika. Hata katika ndoa – uhusiano ulio wa karibu zaidi tena wa muhimu kuliko mahusiano yote ya kibinadamu – bado mapungufu ya mume na ya mke yanasumbuana, si kweli?
Lakini hata kama ni vigumu sana, bado tunafahamu kwamba pendo ni la muhimu sana. Sisi sote tunataka na kuhitaji kupendwa. Lakini ni kwa sababu gani? Je! Lengo la pendo ni lipi? Kusudi lake kubwa ni lipi? Wakati Mungu anatukaribia sisi wanadamu katika mapungufu yetu na makusudi Anataka kufanya nini?
1 Yohana 4:10-12 Hili ndilo pendo, si kwamba sisi tulimpenda Mungu, bali kwamba yeye alitupenda sisi, akamtuma Mwanawe kuwa kipatanisho kwa dhambi zetu. Wapenzi ikiwa Mungu alitupenda sisi hivi, imetupasa na sisi kupendana. Hakuna mtu aliyemwona Mungu wakati wo wote. Tukipendana, Mungu hukaa ndani yetu, na pendo lake limekamilika ndani yetu.
Ni kweli, lengo la pendo la Mungu ni kwamba tulipokee, tusamehewe kulipitia, tulifamahu, tuanze kuelewa kiasi cha upendo wake kwetu. Lakini pia, kuna lengo lingine, sijui kama umeliona?
Tukipendana, Mungu hukaa ndani yetu, na pendo lake limekamilika ndani yetu.
Umpende Mungu. Upende watu wengine.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.