Macho ya Kuona
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Yakobo 1:5 Lakini mtu wa kwenu akipungukiwa na hekima, na aombe dua kwa Mungu, awapaye wote, kwa ukarimu, wala hakemei; naye atapewa.
Ni ajabu, ukitafakari kidogo, jinsi mitazamo yetu hasi na changamoto za zamani vikiunganika na hali ya kubanwa leo vinazidi kupotosha maono yetu … na hii inasababisha tufanye maamuzi yasiyo sahihi na kutuletea madhara. Halafu baada ya kula hasara, hatuelewi kwamba imetokana na maamuzi mabaya tuliyoyafanya hapo awali.
Nina marafiki wawili ambao ni mahakimu. Mmoja katika mahakama ya jamii inayoshughulika na maswala mazito ya talaka na ni nani atakayebaki na watoto. Mwingine katika mahakama ya watoto inayoshughulika na makosa ya jinai yanayotendewa na vijana.
Mimi kabisa, singeweza kufanya kazi yao, kwa sababu mara nyingi, hukumu wanazolazimika kutoa katika ulimwengu wetu usiokamilika, ni kuangalia ni wapi madhara yatakuwa nafuu. Hii inahitaji hekima ya hali ya juu. Ni hekima ambayo watu wa kawaida kama wewe na mimi hatuna.
Lakini tukisema kweli, wewe na mimi tunahitaji hekima – hekima nyingi tu – katika maisha ya kila siku ili tuweze kufanya maamuzi bora yanayoweza kuleta matokeo mazuri.
Yakobo 1:5 Lakini mtu wa kwenu akipungukiwa na hekima, na aombe dua kwa Mungu, awapaye wote, kwa ukarimu, wala hakemei; naye atapewa.
Wakati unahangaika kwa kukosa hekima katika mahusiano fulani, katika kitendawili fulani au tatizo ambalo halitatuliwi, kusikia ahadi hiyo ni habari njema kabisa, si kweli? Moyo wa Mungu, katikati ya vurugu hizo, imejaa ukarimu, imejaa na kufurika na nia ya kutoa, inajaa furaha ya kukukirimia hekima.
Lakini mtu wa kwenu akipungukiwa na hekima, na aombe dua kwa Mungu, awapaye wote, kwa ukarimu, wala hakemei; naye atapewa.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.