Maelekezo ya Kufanya Amani (5)
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Wakolosai 3:17 Na kila mfanyalo, kwa neno au kwa tendo, fanyeni yote katika jina la Bwana Yesu, mkimshukuru Mungu Baba kwa yeye.
Kuwa na amani hakuhusu mambo yanayotupata kutoka kwa watu wengine tu, au mazingira yetu au changamoto za maisha, lakini pia, amani inahusu namna mtu anajielewa na kukubali na kufurahia nafasi yake katika viumbe.
Kujithamini inachangia sana kusababisha mtu kupokea amani ambayo Mungu alikusudia apate. Lakini tunapojilinganisha na watu wengine; warembo, waliofanikisha mambo yao na kuwa na mali, wakiwa pia na ndoa zenye furaha na kuwa na watoto wanaostawi, tunaona mara nyingi kwamba hatufai.
Ninayoweza kufanya na mchango wangu ni vitu vidogo sana, haviwezi kufanya lolote la maana nikijilinganisha na wengine walioko huko.
Ndivyo inavyotokea pale tunapotumia vigezo vya uliwengu huu ili tujipime. Lakini ingekuwaje kama tungekataa kucheza kwa mpigo wa ngoma yao na kujaribu kumpendeza mmoja tu?
Wakolosai 3:17 Na kila mfanyalo, kwa neno au kwa tendo, fanyeni yote katika jina la Bwana Yesu, mkimshukuru Mungu Baba kwa yeye.
Thamani yako, thamani yangu, haitokani na jinsi tunavyojilinganisha na umati wa watu, wala haitokani na jinsi wanavyotuona wao. Tukiishi kwa kumpendeza Mungu basi hapo hakutakuwa na mjadala tena kuhusu thamani yetu kwa sababu tunajua kwamba Yesu alikufa kwa ajili yetu. Hii ndiyo thamani yetu … hii ndiyo thamani yako kubwa!
Kwa hiyo, kila ufanyalo, kwa neno au kwa tendo … lifanye kwa ajili yake. Ishi maisha yako kwa ajili ya Yesu kama Bwana wako. Zidi kufananishwa naye … tena zidi kumwishia yeye.
Na kila mfanyalo, kwa neno au kwa tendo, fanyeni yote katika jina la Bwana Yesu, mkimshukuru Mungu Baba kwa yeye.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.