Mageuzi Makubwa
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Zaburi 107:35 Amegeuza jangwa ikawa ziwa la maji, na nchi kavu ikawa chemchemi za maji.
Kuna wakati tunaona taabu tupu mbele yetu, Lakini ni kwenye vipindi vigumu Mungu ndipo Mungu kwa mtazamo wake huwa anaona fursa kubwa ya kutuletea mabadiliko kuliko tunavyofikiri.
Labda inaonekana kuwa bora kuliko hali halisi ya mambo. Labda unafikiri kwamba ni kama hadithi tu za kizee. Na kama una mashaka hayo, mimi ninakuelewa. Kwasababu, kama ukiwa jangwani halafu akaona dimbwi la maji mbele yake, anaweza kufikiri ni mazingaombo. I sawa?.
Lakini kama utamruhusu Mungu kuingilia kati, atamke neno juu ya mazingira yako ya ukame, basi mambo yako yataanza kubadilika. Yaani kila kitu kinaanza kubadilika.
Zaburi 107:35 Amegeuza jangwa ikawa ziwa la maji, na nchi kavu ikawa chemchemi za maji.
Zaburi hii inahusu mambo ya ajabu Mungu amewatendea watu wake; wakiwa wamepotea, wakiwa wamefungwa, wakiwa wameonewa, wakiwa na njaa na kiu, wakiwa wajinga na kumwasi Mungu na kujiletea taabu wenyewe.
Ungechukua muda kusoma sura yote ya Zaburi hii kwa sababu katika mazingira yoyote mtu angefikiria, moyo wake Mungu umekusudia kuleta ukombozi. Moyo wake unataka kuokoa, kuweka huru na kufariji. Ni Zaburi inayosifu uaminifu endelevu wa Mungu na upendo wake. Ni Zaburi inayohusu uwezo wa Mungu kuleta matengenezo hata ni shida au matatizo gani.
Amegeuza jangwa ikawa ziwa la maji, na nchi kavu ikawa chemchemi za maji.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.