Mambo Ambayo Yesu Hakusema
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Luka 9:23,24 Akawaambia wote, Mtu ye yote akitaka kunifuata, na ajikane mwenyewe, ajitwike msalaba wake kila siku, anifuate. Kwa kuwa mtu atakaye kuiponya nafsi yake ataiangamiza, na mtu atakayeiangamiza nafsi yake kwa ajili yangu ndiye atakayeisalimisha.
Leo, ulimwengu unataka kutwambia kwamba lengo kuu la mwanadamu ni kuishi maisha mazuri na kufurahi. Ni sawa, kwa sehemu, lakini lengo hili lina hatari fulani.
Ukiniuliza kama ninafikiri kwamba Mungu anataka kutubariki jibu langu lingekuwa, Ndiyo, asilimia mia! Ni kweli kabisa! Kama vile baba mzazi anayependa watoto wake, Mungu anatutakia yaliyo bora.
Lakini mtu akipinda dhana hiyo ya mibaraka yake Mungu kwa kuichanganya na lengo lenye ubinafsi la watu wa dunia hii ambalo wanalolieneza kote kote, atajikuta kwamba amepotoshwa kwenda pabaya.
Mbiu wa kutuamsha. Yafuatayo ni maneno ambayo Yesu kamwe hakusema: Sikiliza sauti ya moyo wako. Uwe mwaminifu kwako wewe binafsi. Tegemea hisia zako za ndani. Jisikie kwamba wewe unafaa kama ulivyo. Kilicho muhimu ni kuwa na furaha. Uwe mtu mwema tu.
Hata kama umesikia misemo hiyo mara nyingi na kuvutwa nayo, mawazao hayo hayatokani na mafundisho yake Yesu. Lakini sikiliza kitu kimoja alichokisema Yesu:
Luka 9:23,24 Akawaambia wote, Mtu ye yote akitaka kunifuata, na ajikane mwenyewe, ajitwike msalaba wake kila siku, anifuate. Kwa kuwa mtu atakaye kuiponya nafsi yake ataiangamiza, na mtu atakayeiangamiza nafsi yake kwa ajili yangu ndiye atakayeisalimisha.
Hayo, rafiki yangu, ni kinyume kabisa na ushauri ungeupata kutoka kwa ulimwengu huu kuhusu maisha yako. Kuna uamuzi tunaopaswa kufanya hapo, kila mmoja wetu. Uwe na furaha tu na ujisikie kwamba uko sawa … au chukua msalaba wako na kumfuata Yesu.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.