Mambo Muhimu ya Haraka
Add to FavouritesMhubiri 11:7,8 Kweli nuru ni tamu, tena ni jambo la kupendeza macho kutazama jua. Naam, mtu akiishi miaka mingi, na aifurahie yote; lakini na azikumbuke siku zijazo za giza, kwa maana zitakuwa nyingi. Mambo yote yajayo ni ubatili.
Siku zetu za kuishi hapa duniani – siku zako na siku zangu – zimehesabiwa. Tumebaki na muda mfupi tu wa kutikisa na kuleta mabadiliko kwenye maisha ya watu wanaotuzunguka, watu wakaribu yetu.
Tumekuwa na masimulizi wiki hii kuhusu umuhimu wa kutumia vipawa na rasilimali Mungu alizoweka mikononi mwetu ili tutende mema popote tuendapo. Kweli itatugharimu na inawezekana mazingira yasipendeze mara nyingi kwa sababu ya wasiwasi na mashaka.
Lakini tuseme wazi. Muda tuliobakiza kutenda yale mema ambayo Mungu ametuitia unazidi kupungua kila sekunde. hata kama tunaishi kwenye dunia inayotumia vipimo vya urefu, upana na kimo, bado kuna kipimo kingine cha nne tunachopaswa kukitumia, yaani muda wa siku, miezi na miaka, ambacho tunapenda kukisahau.
Mhubiri 11:7,8 Kweli nuru ni tamu, tena ni jambo la kupendeza macho kutazama jua. Naam, mtu akiishi miaka mingi, na aifurahie yote; lakini na azikumbuke siku zijazo za giza, kwa maana zitakuwa nyingi. Mambo yote yajayo ni ubatili.
Kama umemwamini Yesu, basi utaishi milele pamoja naye. Tutamwabudu milele, Lakini pia ina maana kwamba fursa tuliyo nayo ya kutenda mema na kusaidia watu wengine tukisukumwa na upendo wake na kuona watu wakiokoka kwa kumjua yeye, muda ule utakuwa umeisha.
Ina maana kwamba kuna hisia fulani ya haraka kukamilisha yaliyo muhimu. Ni kweli, inapendeza kuishi na kutazama jua na kufurahia kila siku ya maisha yetu. Lakini tuwe tunajishughulisha na kazi yake ya kutenda mema popote tuendapo, kabla hatujapitwa na wakati.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.