... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Kuangalia Mambo kwa Upana

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Mhubiri 11:5,6 Kama vile wewe usipojua njia ya upepo ni ipi, wala jinsi mifupa ikuavyo tumboni mwake mja mzito; kadhalika huijui kazi ya Mungu, afanyaye mambo yote. Asubuhi panda mbegu zako, wala jioni usiuzuie mkono wako. Kwa maana wewe hujui ni zipi zitakazofanikiwa, kama ni hii au hii, au kama zote zitafaa sawasawa.

Listen to the radio broadcast of

Kuangalia Mambo kwa Upana


Download audio file

Labda Mungu amekuita ujitolee kwa ajili ya kazi fulani fulani.  Pengine ni kuwezesha kazi zake, au kutoa muda wako na nguvu zako kwa ajili ya huduma fulani au kusaidia mtu fulani.  Haijalishi ni kazi gani, daima itakugharimu.

Kuna jambo fulani ambalo huwezi kulikwepa kama ukitaka kumfuata Yesu.  Lazima itakugharimu kujishughulisha na kazi zake za kuonyesha upendo wake na kushirikisha wengine habari njema.  Ndio maana inawawia wengine vigumu.  Ndio maana tunasita-sita, ndio maana wengine wanasalimu amri na kuacha. 

Yaani hizo ni gharama za awali.  Kuwekeza uchumi pale ambapo kuna hatari bila uhakika kwamba mtu atapata matokeo mazuri yanayolingana na uwekezaji wake.  Uwezekano wa matokeo mazuri ya kuridhisha unaweza kulingana na namna mtu anavyojitolea kuwekeza mali?  Hilo ndilo swali nyeti.  Lakini kwa kazi ya Mungu, swali hilo si sahihi hata kidogo.  Sababu ukiuliza hivyo, utakuwa umesahau uwepo wa Mungu na namna anavyowajibika na kazi zake katika wito aliokuitia. 

Mhubiri 11:5,6  Kama vile wewe usipojua njia ya upepo ni ipi, wala jinsi mifupa ikuavyo tumboni mwake mja mzito; kadhalika huijui kazi ya Mungu, afanyaye mambo yote.  Asubuhi panda mbegu zako, wala jioni usiuzuie mkono wako.  Kwa maana wewe hujui ni zipi zitakazofanikiwa, kama ni hii au hii, au kama zote zitafaa sawasawa. 

Napenda mfano huu wa kuamka alfajiri kwa lengo la kupanda mbegu na kuendelea kufanya kazi mpaka jioni.  Kwa maneno mengine, acha kuahirisha-ahirisha ndugu.  Jitoe muhanga katika wito wa Mungu kwa nguvu zako zote, kwa furaha na bidii. 

Kwa sababu kama kweli amekuitia kazi fulani, basi atakuwa pamoja nawe.  Yeye atasababisha mambo yafanyike.  Kwahiyo, sogea nyuma kidogo, tazama picha yote kwa upana wake, halafu anza kazi! 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.