... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Kuna Mambo Unaweza Kuwa na Uhakika Nayo, Lakini …

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Mhubiri 11:3,4 Mawingu yakiwa yamejaa mvua, yataimimina juu ya nchi; na mti ukianguka kuelekea kusini, au kaskazini, paangukapo ule mti, papo hapo utalala. Mwenye kuuangalia upepo hatapanda; naye ayatazamaye mawingu hatavuna.

Listen to the radio broadcast of

Kuna Mambo Unaweza Kuwa na Uhakika Nayo, Lakini …


Download audio file

Kinachotuwia vigumu mno ni kuanza kupiga hatua ya imani wakati mazingira yetu ni ya wasiwasi.  Ni vigumu kuwekeza muda wetu, nguvu yetu na rasilimali zetu kuanzisha huduma nzuri wakati matokeo yake hayana uhakika.

Kama vile msemo unaosema, “Mtu hawezi kuwa na uhakika wowote maishani kuhusu lolote lile, isipokuwa mambo mawili: kifo na kodi.”  Mengine yote ni kama kubahatisha tu.  Na kama vile tulivyoona jana, hata baraka za maisha zinazoonekana kuwa imara kama vile, ndoa, nyumba, siku moja zote zitaisha. 

Kwahiyo, katikakati ya wasiwasi zote hizo, utasikia kwamba Mungu amekusukuma kujitolea, uwekeze kwenye kazi fulani njema.  Lakini inaonekana kwamba si muda mwafaka.  Mazingira yanatatanisha ,Kwahiyo, tunachokifanya mara nyingi ni kuwaza moyoni na kusema, “Acha niahirishe kwanza.” 

Mhubiri 11:3,4  Mawingu yakiwa yamejaa mvua, yataimimina juu ya nchi; na mti ukianguka kuelekea kusini, au kaskazini, paangukapo ule mti, papo hapo utalala.  Mwenye kuuangalia upepo hatapanda; naye ayatazamaye mawingu hatavuna. 

Ina maana, Mungu anataka tuanze kupiga hatua kwa imani, mara zote, mazingira hayawezi kuridhisha.  Daima kuna wasiwasi fulani inayotokana na mtazamo wetu finyu wa ki-dunia.  Lakini kama mtu atasubiri hadi mazingira yawe mazuri basi hataanza kupiga hatua. 

Umwamini Mungu.  Piga hatua licha ya mazingira yako. 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.