Mambo Yanayovunja Moyo
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
1 Petro 5:10 Na Mungu wa neema yote, aliyewaita kuingia katika utukufu wake wa milele katika Kristo, mkiisha kuteswa kwa muda kidogo, yeye mwenyewe atawatengeneza, na kuwathibitisha, na kuwatia nguvu.
Mateso ni kitu kati ambayo yanaweza kuharibu imani ya mtu kwa urahisi. Je! Mungu wa upendo angewezaje kuruhusu upitie mambo mazito kama hayo?
Kama itawezekana, ningependa leo kukuomba utulie, ukae chini na kutafakari kipindi kigumu cha mateso uliowahi kukipitia maishani mwako. Kile kitu kimoja, uhusiano ule mmoja uliovunjika, hali ile ngumu iliyotaka kukupasua na kidogo kukuangamiza.
Najiuliza, ukitafakari hayo na kujilinganisha ulivyo leo hii na jinsi ulivyokuwa kabla ya mateso yale makubwa, je! Umebadilika kiasi gani?
Mateso yamegusaje tabia yako? Je yamekushushaje imani yako? Yamekufanya kuwa mpole, kuwa mtu anayechukiwa na wengine? Yamekushusha na kukunyenyekeza? Je! Mateso yamekurithisha vitu gani?
1 Petro 5:10 Na Mungu wa neema yote, aliyewaita kuingia katika utukufu wake wa milele katika Kristo, mkiisha kuteswa kwa muda kidogo, yeye mwenyewe atawatengeneza, na kuwathibitisha, na kuwatia nguvu.
Mungu anayo tabia ya kutengeneza mambo , hutengeneza tabia zetu kutengeneza maadili mema, kwa kututia nguvu, kututegemeza, kututhibitisha, akitukirimia neema yake … huko akitubeba kuelekea hatima yetu, yaani kuingia katika utukufu wake wa milele.
Kujua haya, kwa kweli kutakubadilisha, lazima ubadilishwe. Ndiyo maana mara nyingi kinachokuvunja moyo ndicho kinachotengeneza mtazamo wako.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.