Familia Iliyovurugika
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Mwanzo 3:11-15 Akasema, Ni nani aliyekuambia ya kuwa u uchi? Je! Umekula wewe matunda ya mti niliyokuagiza usiyale? Adamu akasema, Huyo mwanamke uliyenipa awe pamoja nami ndiye aliyenipa matunda ya mti huo, nikala. BWANA Mungu akamwambia mwanamke, Nini hili ulilolifanya? Mwanamke akasema, Nyoka alinidanganya, nikala. BWANA Mungu akamwambia nyoka, Kwa sababu umeyafanya hayo, umelaaniwa wewe kuliko wanyama wote, na kuliko hayawani wote walioko mwituni; kwa tumbo utakwenda, na mavumbi utakula siku zote za maisha yako; nami nitaweka uadui kati yako na huyo mwanamke, na kati ya uzao wako na uzao wake; huo utakuponda kichwa, na wewe utamponda kisigino.
Unaweza kuwasikiliza wahubiri kama tulivyoongea habari ya familia kamilifu ya kikristo na namna inavyopaswa kuwa. Lakini je!, Itakuaje kwa familia zilizovurugika? Itakuaje kwa familia zilizovunjika tayari?
Na kweli familia zenye matatizo makubwa zipo nyingi na kama wewe unaifahamu mojawapo basi ujumbe wa leo utakufaa. Mambo yote yalikuwa shwari kwa ajili ya Adamu na Hawa hadi siku walipoasi na kula matunda ya mti ule mmoja waliokuwa wameagizwa wasile.
Mwanzo 3:11-15 Akasema, Ni nani aliyekuambia ya kuwa u uchi? Je! Umekula wewe matunda ya mti niliyokuagiza usiyale? Adamu akasema, Huyo mwanamke uliyenipa awe pamoja nami ndiye aliyenipa matunda ya mti huo, nikala. BWANA Mungu akamwambia mwanamke, Nini hili ulilolifanya? Mwanamke akasema, Nyoka alinidanganya, nikala. BWANA Mungu akamwambia nyoka, Kwa sababu umeyafanya hayo, umelaaniwa wewe kuliko wanyama wote, na kuliko hayawani wote walioko mwituni; kwa tumbo utakwenda, na mavumbi utakula siku zote za maisha yako; nami nitaweka uadui kati yako na huyo mwanamke, na kati ya uzao wako na uzao wake; huo utakuponda kichwa, na wewe utamponda kisigino.
Dhambi inatenganisha na kupasua familia. Tunapomkataa Mungu na kuamua kwenda kwa njia yetu wenyewe, matokeo juu ya familia zetu ni mabaya mno.
Hatua yoyote ile mmeyofikia kwenye familia yako, humuwezi kubadilisha yaliyopita, lakini mnaweza kutumaini kuandaa yaliyo bora huko mbeleni. Unaweza kuamua sasa hivi hapo ulipo kujishusha na kuacha kiburi na kumheshimu Bwana Mungu wako kila wakati unapovuta pumzi.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.