... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Matamshi Hasi Yanamharibu Mtu kwa Ndani

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Zaburi 19:14 Maneno ya kinywa changu, na mawazo ya moyo wangu, yapate kibali mbele zako, Ee BWANA, Mwamba wangu na Mwokozi wangu.

Listen to the radio broadcast of

Matamshi Hasi Yanamharibu Mtu kwa Ndani


Download audio file

Sisi sote tuna masimulizi tunayoyafanya nafsini mwetu.  Tunatengeneza hadithi za maisha yetu na tunarudia-rudia masimulizi yale  yale hadi pale yanapotikisa maisha yetu na kututambulisha pia.

Kama mtu aliambiwa tangu utoto wake kwamba ni mpumbavu, unaweza kuwa na uhakika kwamba hata kama si kwa sura ya nje, ndani anajiambia tena na tena kwamba hafai, kwamba ni mpumbavu. 

Najiuliza, ni masimulizi gani hasi, au picha gani potovu uliyowekewa kichwani na moyoni mwako ambavyo vinakuharibia baraka zote Mungu alizokuwa ameandaa kwa ajili yako.  Mwanasaikolojia yeyote atakwambia kwamba masimulizi hayo mabaya ya ndani, ni vigumu sana mtu kuwekwa huru na kwa wengine  wanzsema haiwezikani kabisa. 

Kama wewe unatatizwa na mtazamo hasi kama huo, unachokihitaji ni kitu kimoja – uwezo, uwezo wa ki-Mungu, uwezo wa Roho Mtakatifu ili uwekwe huru.  Sasa leo, kwa moyo wangu wote, ninaamini kwamba Mungu anataka kukukirimia uwezo huo.  Sikiliza: 

Zaburi 19:14  Maneno ya kinywa changu, na mawazo ya moyo wangu, yapate kibali mbele zako, Ee BWANA, Mwamba wangu na Mwokozi wangu. 

Kuna uwezo ndani ya Neno la Mungu kwasababu yeye ni Mwamba wako; yeye ndiye akuokoaye.  Ukimwendea na kuomba, Maneno ya kinywa changu, na mawazo ya moyo wangu, yapate kibali mbele zako – atajibu dua yako. 

Roho yake pamoja na Neno lake vitaachia uwezo ndani yako, uwezo wa kukubadilisha, uwezo wa kufanya ukweli ufukuze masimulizi potovu yaliyokuwa yanakuua pole pole.

Maneno ya kinywa changu, na mawazo ya moyo wangu, yapate kibali mbele zako, Ee BWANA, Mwamba wangu na Mwokozi wangu.  

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.


We use cookies to improve your browsing experience, analyse site traffic & personalise content, but we do not track you when you leave this site. To find out how we utilise & protect your data, check out our "Privacy Policy".

Privacy Policy