Matazamio Yasiyowezekana
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Yohana 16:33 Hayo nimewaambieni mpate kuwa na amani ndani yangu. Ulimwenguni mnayo dhiki; lakini jipeni moyo; mimi nimeushinda ulimwengu.
Sasa hivi una matazamio gani huko mbeleni? Bila shaka unatazamia yaliyo mema, si kweli? Labda uwekwe huru kutoka kwenye matatizo uliyonayo sasa. Lakini mara nyingi mambo hayatokei kama tunavyotarajia sisi, au unasemaje wewe?
Yaani Kuna vitu vinachekesha kweli, Watu wanatapeliwa mitandaoni kwa kubashiriwa yatakayokuja. Juzi tu hapa niliona tangazo likisema kuna mambo manne ya ajabu yatamtokea mtu Fulani, atapata nyumba mpya, gari mpya, pesa tele na maisha yenye furaha. Mmm, Hivi ni kweli?
Lakini, hiyo si ndoto ya mioyo yetu sote? wakati mambo yanapozidi kutuharibikia, tunaanza kusononeka na kufadhaika!
Angalia, inawezekana unapitia kipindi kizuri mno. Hongera sana. Lakini maisha haikamiliki hivyo daima. Ni mara haba yote yanakusanyikia kwa jinsi ya kukupendeza asilimia mia, hata.
Kwahiyo ukiwa na matazamio ambayo kwa kawaida hayawezi kutarajiwa, inasaidia kujua kwamba Yesu ni mtu afahamuye uhalisia wa mambo. Siku zile akikaribia kusulubiwa – wanafunzi wake walihofia uhai wao –Yesu aliwaambia hivi:
Yohana 16:33 Hayo nimewaambieni mpate kuwa na amani ndani yangu. Ulimwenguni mnayo dhiki; lakini jipeni moyo; mimi nimeushinda ulimwengu.
Hapo ndipo unaweza kupokea ahadi ya kusimamia: duniani utapata matatizo na dhiki. Utabanwa mno na mazingira ya ulimwengu huu. Haleluya! Ila, unaweza kuimarika. Kwanini? Kwa sababu tayari, Yesu ameshaushinda ulimwengu na yote yaliyomo.
Hayo nimewaambieni mpate kuwa na amani ndani yangu.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.