Mimi Mwenye Hamaki, Wewe Mwenye Hamaki
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
1 Wakorintho 13:5 Upendo haukosi kuwa na adabu; hautafuti mambo yake; hauoni uchungu; hauhesabu mabaya.
Kuna siku mimi ni mwenye hamaki, kuna siku hata wewe unakuwa mwenye hamaki. Sote tunaweza kuwa wenye harara. Natumaini kwamba hali hiyo haitokei mara nyingi, lakini hua inatokea. Je! Unatendaje wakati una hali hiyo? Je! Watu wengine wanakuonaje?
Sisi sote tunaelewa jinsi mtu anajisikia akiwa karibu ya mtu mwenye hamaki. Haipendezi na tukisema ukweli, tunajitahidi kujiepusha naye haraka iwezekanavyo.
Lakini ni mara chache tunavyoweza kufikiria wanavyojisikia wengine wakati ni sisi ndiyo wenye hamaki. Tunachokijua tu ni kwamba sisi ndiyo tumesumbuliwa na wengine, lazima watupishe. Yaani hatujitambui tena. Sasa wakati utajikuta katika hali hiyo ya kuchukiza huko mbeleni, jaribu kujipima na maneno yafuatayo:
1 Wakorintho 13:5 Upendo haukosi kuwa na adabu; hautafuti mambo yake; hauoni uchungu; hauhesabu mabaya.
Katika mstari huu tunapata dalili nne ya mwenye hamaki: anakosa adabu, ana ubinafsi, ni mwepesi wa hasira bila kusahau kutaja kwamba anakuwa na kinyongo moyoni kutokana na tukio liliomsababisha awe na hamaki hapo mwanzo.
Je! Niko sahihi? Si ndivyo tulivyo wakati tuna hamaki?
Lakini kufuatana na Neno la Mungu, upendo hauna tabia kama hiyo. Haukosi kuwa na adabu; hautafuti mambo yake; hauoni uchungu; hauhesabu mabaya.
#Tujikumbushe: Nikumbuke wakati nitajisikia kuwa na hamaki mara tena, kwamba upendo haufanani na hali hiyo. Lazima niwapende wale ambao Mungu amenipa niwapende.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.