Moyo Wake wa Ukombozi
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Zaburi 28:1,2 Ee BWANA, nitakuita wewe, mwamba wangu, usiwe kwangu kama kiziwi. Nisije nikafanana nao washukao shimoni, ikiwa umeninyamalia. Uisikie sauti ya dua yangu nikuombapo, nikipainulia patakatifu pako mikono yangu.
Kila wakati Mungu anatuita ili tumtendee jambo fulani, ndani yetu kuna hisia ambayo haitaki kusumbuliwa bali inataka kuendelea kukaa katika starehe. Yaani, kuna uzito fulani, upinzani, na hofu kwa kufikiria tutakavyogharimiwa.
Kama wewe umemwamini Yesu lakini hujasikia hata siku moja ule uzito, ule upinzani wa ndani, ile hofu kwa yale Yesu amekuitia uyafanya, kwa kweli kuna shida kubwa. Kwa sababu yeye hatafuti waamini wanaopenda starehe, bali anatafuta wanafunzi walio tayari kuchukua msalaba wake na kumfuata popote pale atakapowongoza ili awajibike katika kazi ya kupenda na kuokoa ulimwengu uliopotea na ulimwengu unaoumia.
Mfalme Daudi alipitia njia ngumu hadi kumilikishwa kwenye kiti cha enzi ya Israeli. Aliyaona mengi ya kutisha, alinusurika mara kwa mara wakati watu walijaribu kumwangamiza lakini kama asingalifuata wito wa Mungu, sijui ingalikuwaje kwa kuwa Yesu baada ya miaka elfu moja, alizaliwa moja kwa moja kupitia ukoo wake.
Kipindi kimoja kilichotisha, Daudi alimlilia Mungu hivi:
Zaburi 28:1,2 Ee BWANA, nitakuita wewe, mwamba wangu, usiwe kwangu kama kiziwi. Nisije nikafanana nao washukao shimoni, ikiwa umeninyamalia. Uisikie sauti ya dua yangu nikuombapo, nikipainulia patakatifu pako mikono yangu.
Bruce Wilkinson, katika kitabu chake kiitwacho “Sala ya Yabez” aliandika hivi: “Daima mtu atakuwa na hofu akianza kumiliki eneo jipya kwa ajili ya Mungu, lakini pia, atasikia furaha kuu akiona jinsi Mungu anavyombeba katika jitihada hiyo.”
Na kwa kweli, ni furaha kuu kabisa usikwamishwe na hofu. Mfuate Yesu popote atakapokuongoza kwani atakusikia ukimlilia na atakuhurumia.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.