Msingi Imara
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Mithali 3:5-8 Mtumaini BWANA kwa moyo wako wote, wala usizitegemee akili zako mwenyewe; katika nija zako zote mkiri yeye, naye atayanyosha mapito yako. Usiwe mwenye hekima machoni pako; mche BWANA, ukajiepushe na uovu. Itakuwa afya mwilini pako, na mafuta mifupani mwako.
Ikiwa uko kama mimi, bila shaka, utakuwa umeshakuwa na mpango kwa ajili ya mwaka huu mpya. Mambo unavyotaka uyatimize. Likizo unayotaka kupata. Mahusiano unayotaka kuyaboresha. Mambo kama hayo.
Mtu anaweza kupanga kila kitu kupita kiasi au anaweza kuzembea kwa kutokupanga kwa kutosha kwa ajili ya mwaka mpya. Inategemeana na tabia ya mtu. Yote mawili ni makosa. Kupanga kupita kiasi kunaonyesha kiburi fulani kwamba tunaweza kutabiri mambo yajayo. Kutokupanga pia kunaonyesha uvivu kwasababu kuna mambo mengine yako ndani ya uwezo wetu na inapasa tuwajibike.
Lakini hata uwe upande gani leo ninataka kukupa andiko linaloweza kukupa msingi uliowekwa kwenye mwamba imara kwa ajili ya maisha yako ya mwaka huu.
Mithali 3:5-8 Mtumaini BWANA kwa moyo wako wote, wala usizitegemee akili zako mwenyewe; katika nija zako zote mkiri yeye, naye atayanyosha mapito yako. Usiwe mwenye hekima machoni pako; mche BWANA, ukajiepushe na uovu. Itakuwa afya mwilini pako, na mafuta mifupani mwako.
Ukweli ni kwamba, kwenye maisha; pale tusipoweza kutabiri yatakayetokea,– sera ya busara kabisa – ni kumtegemea Bwana kwa moyo wako wote, kuliko kutegemea akili zako mwenyewe. Na ukimtanguliza na kumheshimu kwa kumpa nafasi ya kwanza kwa, yeye mwenyewe atajishughulisha na mambo yako na kuhakikisha kwamba mambo yanaenda sawa kama inavyotakiwa.
Haijalishi maisha yako yatakuwa na matatizo gani mwaka huu, ukimcha BWANA, na kujiepusha na uovu, itakuwa afya mwilini pako, na mafuta mifupani mwako.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.