Msingi wa Amani Nyumbani
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Mwanzo 2:24 Kwa hiyo mwanamume atamwacha baba yake na mama yake naye ataambatana na mkewe, nao watakuwa mwili mmoja.
Kuwa ndani ya familia yenye upendo ni baraka kubwa, si kweli? Lakini hata kama uko ndani ya familia yenye upendo, bado ni kazi kulinda amani. Migongano haikosekani. Kuna mvutano. Na familia zingine, hatimaye zinavunjika.
Tunachokitamani zaidi ni kuwa na amani nyumbani. Ukiwa kibaruani na kufanya shughuli za kila siku, tayari unabanwa na mambo mengi kazini, migogoro unayokutana nayo inakutosha kabisa.
Sasa ukirudi nyumbani na kuingia ndani, unachokitafuta ni amani. Unataka kukaribishwa vizuri nyumbani kwako. Unataka kuburudishwa, kutulia na kupumzika. Sisi sote tunataka iwe hivi, lakini kuna wakati haitokei jamani.
Kwa hiyo, leo ninataka turudi kwenye misingi. kwa sababu swala la kuwa familia na kuishi vizuri pamoja ni nguzo imara zinazoshikilia mambo mengine yote ya jamii.
Mwanzo 2:24 Kwa hiyo mwanamume atamwacha baba yake na mama yake naye ataambatana na mkewe, nao watakuwa mwili mmoja.
Kwa mawazo ya watu wengi siku hizi, dhana ya ndoa imewekwa pembeni kabisa. Wasio wachache wanaona kwamba ni taasisi iliyopitwa na wakati. Lakini ndoa ilikuwa mpango wa Mungu daima, tangu mwanzo kwa wengi wetu, sisemi kwa kila mtu kwa sababu wengine wachache hawaoi au hawaolewi.
Nguvu ya kifungo kati ya mume na mke, ni jinsi wanajaliana na kuheshimiana, ndiyo msingi wa nyumba yenye amani. Ninyi waume, na ninyi wake, lazima mjaliane. Mungu aliwafanya ninyi wawili kuwa mmoja. Tangu mwanzo ulikuwa mpango wake.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.