Msingi wa Kujitoa
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Wafilipi 2:3-5 Msitende neno lo lote kwa kushindana wala kwa majivuno; bali kwa unyenyekevu, kila mtu na amhesabu mwenziwe kuwa bora kuliko nafsi yake. Kila mtu asiangalie mambo yake mwenyewe, bali kila mtu aangalie mambo ya wengine. Iweni na nia iyo hiyo ndani yenu ambayo ilikuwamo pia ndani ya Kristo Yesu.
Kuna mabadiliko makubwa yanayofanyika kwenye mitazamo ya watu, mtazamo ambayo haikuanzia leo. Ni kama dunia nzima inatoka kwenye mtazamo wa umma na ushirikiano kwenda kwa mtazamo wa ubinafsi.
Nchi za magharibi kadiri uchumi ulivyokuwa unaendela sana karne zile zilizopita, na kadiri mapato ya wananchi yalivyozidikupanda, na komputa zenye nguvu zilivyokuwa zintengenezwa kila siku kiasi kwamba hadi leo mtu anaweza kuishika kompyuta mikononi mwake; au ndani ya simu yake janja, hivyo ndivyo ubinafsi ulivyozidi kurarua jamii zetu na kufanya mtu kujiona kama anastahili kupewa kila kitu anachohitaji. Hali hii imedhihirika na iko wazi sana
Halafu sasa, kwa nchi zinazotajwa kuwa zinaanza kupata maendeleo, watu wao wamesha-ambukizwa mtazamo huo wa ubinafsi;.. uliotoka magharibi, na wao sasa wanaanza kutawaliwa na madai kwamba; kila mtu anastahili kupata hiki na kile.
Mzizi wa ubinafsi tumekuwa nao tangu enzi za kale. Ndio maana wito wa Yesu kuishi maisha ya kujitoa kwa ajili ya wengine, daima umeenda kinyume na utaendelea kuwa kinyume na utamaduni. Ndio maana wito wa Yesu kumfuata katika maisha ya kujitolea, watu wengi wanachukizwa nao.
Wafilipi 2:3-5 Msitende neno lo lote kwa kushindana wala kwa majivuno; bali kwa unyenyekevu, kila mtu na amhesabu mwenziwe kuwa bora kuliko nafsi yake. Kila mtu asiangalie mambo yake mwenyewe, bali kila mtu aangalie mambo ya wengine. Iweni na nia iyo hiyo ndani yenu ambayo ilikuwamo pia ndani ya Kristo Yesu.
Kama tunavyojua, hata kama yeye alikuwa Mwana wa Mungu, alikubali kuacha yote ili afanyike kuwa mmoja wetu, na kusulubiwa kisha kufa, kwa ajili yetu. Kweli, tumezungukwa na ulimwengu unaozidi kutawaliwa na mtazamo wa ubinafsi na wa kudai haki. Lakini maisha ya mfuasi wa Kristo ni kinyume kabisa na mtazamo huo, ujue hilo.
Iweni na nia iyo hiyo ndani yenu ambayo ilikuwamo pia ndani ya Kristo Yesu.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.