Msingi wa Umilele
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
2 Wakorintho 4:16-18 Kwa hiyo hatulegei; bali ijapokuwa utu wetu wa nje unachakaa, lakini utu wetu wa ndani unafanywa upya siku kwa siku. Maana dhiki yetu nyepesi, iliyo ya muda wa kitambo tu, yatufanyia utukufu wa milele uzidio kuwa mwingi sana; tusiviangalie vinavyoonekana, bali visivyoonekana. Kwa maana vinavyoonekana ni vya muda tu; bali visivyoonekana ni vya milele.
Ni kipi kinakusukuma kuendelea na mahangaiko ya maisha ya kila siku ukikumbana na magumu mara kwa mara? Je! Unatazamia kuona nini? Je! Una matumaini kitu gani ya baadaye?
Sisi ni wageni na wasafiri hapa duniani. Tukipambana na maisha, siku baada ya siku, miili yetu inazeheka na kuelekea kaburini.
Usinielewe vibaya. Mimi ninafurahia maisha; na ninaamini na hata wewe unayafurahia. Lakini daima kuna matatizo na changamoto, si kweli? Kwa hiyo; nataka kujua pale ulipofikia katika safari yako, je! Ni tumaini gani la baadaye linalokupa nguvu za kuendelea? Akiwa katika dhiki kuu, Mtume Paulo aliweza kutuambia hivi:
2 Wakorintho 4:16-18 Kwa hiyo hatulegei; bali ijapokuwa utu wetu wa nje unachakaa, lakini utu wetu wa ndani unafanywa upya siku kwa siku. Maana dhiki yetu nyepesi, iliyo ya muda wa kitambo tu, yatufanyia utukufu wa milele uzidio kuwa mwingi sana; tusiviangalie vinavyoonekana, bali visivyoonekana. Kwa maana vinavyoonekana ni vya muda tu; bali visivyoonekana ni vya milele.
Kilichomwezesha Paulo kuendelea kupambana ni kipi? Ni kujua hakika kwamba; visivyoonekana; yaani vya milele; siku moja vitakua vyake. Rafiki yangu, Yesu alikuja kwa ajili yako. Alikufa na kufufuka tena kwa ajili yako. Umwamini yeye kwa moyo wako wote … halafu ujue haya – kwamba uzito wa utukufu unaokungojea unazidi sana yale yote unayotamani. endelea na safari.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.