... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Mtazamo Tofauti Kabisa

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

1 Petro 1:24,25 Maana, mwili wote ni kama majani, na fahari yake yote ni kama ua la majani. Majani hukauka na ua lake huanguka; bali Neno la Bwana hudumu hata milele. Na neno hilo ni neno lile jema lililohubiriwa kwenu.

Listen to the radio broadcast of

Mtazamo Tofauti Kabisa


Download audio file

Inazidi kuwa ngumu kwa mtu anayemwamini Yesu kuendelea kuamini Biblia.  Labda mahali ulipo, utasema ni kweli.  Eti, sehemu nyingi za Biblia imepitwa na wakati.  Lakini mimi, siwezi kukubaliana na wewe.

Vitabu 66 ambavyo viko ndani ya Biblia viliandikwa na watu mbali mbali, katika mazingira tofauti tofauti kupitia miaka 1,500.  Wakati ilikuwa inaandikwa na kwa miaka mingine 2,000, daima watu wameipinga kabisa.

Watu wa Mungu wenyewe, Waisraeli walikataa manabii Mungu aliyetuma kwao.  Isitoshe, walimsulubisha Yesu, Mwana wa Mungu.  Kanisa lenyewe katika historia yake limewahi kupinga Biblia.  Mfano: wakati viongozi walimchoma moto William Tyndale mwaka wa 1536 kwa sababu alitafsiri Biblia kutoka Kilatini kuiweka katika Kiingereza.

Kwa kweli, Neno la Mungu limepitia magumu mengi, lakini bado tuko nalo.  Bado linaendelea kushinda.  Kwa nini?

1 Petro 1:24,25  Maana, mwili wote ni kama majani, na fahari yake yote ni kama ua la majani.  Majani hukauka na ua lake huanguka; bali Neno la Bwana hudumu hata milele.  Na neno hilo ni neno lile jema lililohubiriwa kwenu.

Mimi ninakubaliana kabisa na mwanateolojia akiwa pia mchungaji aitwaye R.C. Sproul wakati aliandika hivi:  “Hatuwezi kuchunguza andiko la Biblia kwa mtazamo wetu wa karne ya 21 na kubadili maana yake.  Kama mtazamo wa karne ya 21 hauendani na Biblia, basi mtazamo ule si sahihi, si kwamba Biblia imekosea.”

Majani hukauka na ua lake huanguka; bali Neno la Bwana hudumu hata milele.    

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.


We use cookies to improve your browsing experience, analyse site traffic & personalise content, but we do not track you when you leave this site. To find out how we utilise & protect your data, check out our "Privacy Policy".

Privacy Policy