... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Muda Ukiwadia

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

1 Mambo ya Nyakati 28:10 Jihadhari basi; kwani BWANA amekuchagua wewe ili ujenge nyumba itakayokuwa mahali patakatifu; uwe hodari ukatende hivyo.

Listen to the radio broadcast of

Muda Ukiwadia


Download audio file

Sisi sote tunayo matazamio na ndoto.  Siku moja hiki kitatokea … siku moja, kile nacho kitatokea … na mawazo kama hayo ni mazuri.  Mungu anatenda kazi kwa nguvu kupitia maono na ndoto.  Lakini siku moja, muda mwafaka unafika wa kuanzia na kuyaweka katika utendaji.

Kuota ndoto katika fikra zetu kunapendeza.  Yaani uko huru kabisa kuzungukia kote kote katika mawazo yako, kufikiria maajabu yote utakayoyatenda … siku moja; wakati unaofaa; wakati yote yatakuwa yameoanishwa vizuri.

Ni kweli, mtu anaweza kuwa mtu anayeota vizuri, lakini kuanza kazi kabisa na kutumia nguvu zake mara nyingi ni kama hakupendezi.  Yaani ni maudhi.  Ni kazi ngumu kabisa.  Anasema, Nitasubiri kwanza muda mwafaka.  Unaona, mtu akiangalia ukubwa wa kazi iliyopo, mara nyingi anaahirisha na kusema bado, muda mwafaka haujafika.

Mfalme Daudi alimwambia mwanae Sulemani, atakayeshika nafasi yake kwenye kiti cha enzi, akasema hivi:

1 Mambo ya Nyakati 28:10  Jihadhari basi; kwani BWANA amekuchagua wewe ili ujenge nyumba itakayokuwa mahali patakatifu; uwe hodari ukatende hivyo.

Kama utaendelea kusoma habari ya mipango ya Daudi aliyopewa ramani ya jengo, utaelewa kwamba ilikuwa kazi kubwa mno.  Kumbuka kwamba wakati ule hawakuwa na mashine za kurahisisha kazi, wala umeme na kadhalika.

Inawezekana muda hautaonekana kuwa ni mwafaka.  Mazingira mara nyingi hayawezi kuwa mazuri asilimia mia.  Lakini kama Mungu amekuagiza kazi yo yote ile, hata kama ni kubwa mno, inabidi hatimaye, kupiga hatua na kuanza.  

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.